Jumatatu, 12 Desemba 2016

TAASISI YA AGRI-BUSNESS MEDIA INNITIATIVE YASHIRIKI UZINDUZI WA UNGA WA VIAZI LISHE JIJINI MWANZA

Posted by Esta Malibiche on Dec 12,2016


Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ) yenye makazi yake Jijini Mwanza, Deborah Mallaba, akizungumza kwenye uzinduzi wa Unga wa Viazi Lishe uliofanyika hii leo Jijini Mwanza. Taaisisi hiyo imekuwa ikiwaunganisha wakulima na wataalamu wa kilimo kupitia vyombo vya habari.
Unga wa viazi lishe ni muhimu kiafya kwani una wingi wa vitamini A miongoni mwa vitamini mbalimbali ambapo husaidia kuondokana na matatizo ya kuona (upofu). Pia viazi hivyo hutumika kama chakula, na unga wake ni bora kwa ajili ya utengenezaji wa mandazi, chapati, keki, biskuti na vitafunwa vya kila aina.
Taasisi hiyo imeshirikia kama miongoni mwa taasisi hususani za wajasiriamali wanawake zinazojihusisha na kilimo ikiwemo mbogamboga na matunda. Lengo lake ni kuhakikisha wanawake wanajiinua kiuchumi ili kuondokana na utegemezi na hatimaye kuondoana na adha zinazoweza kuwakumba ikiwemo ukatili kutokana na utegemezi.
Uzinduzi huo umeenda pamoja na Kilele cha Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia Duniani, yaliyoanza Novemba 25,2016 hadi leo Disemba 10,2016.
Na BMGHabari

Mgeni rasmi ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu mkoani Mwanza, Kiteto Zawadi Koshuma, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Unga wa Viazi Lishe, uliotayarishwa na wanawake wajasiriamali kutoka Shirika la Sauti ya Wanawake lililopo Ukerewe mkoani Mwanza. 
Shirika hilo limefanikiwa kwenye usindikaji wa bidhaa za kilimo ikiwemo mbogamboga na matunda kwa msaada wa Shirika la Akina Mama Lishe la Tanzania Entrepreneurs Development and Advocacy Organization TEDA.

Akina mama wajasiriamali mkoani Mwanza wakimsikiliza mgeni rasmi, Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Mwanza, Kiteto Zawadi Koshuma, wakati akizindua Unga wa Viazi Lishe hii leo Jijini Mwanza.
Koshuma amewahimiza akina mama kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda ikiwemo viazi lishe kwani soko lake ni kubwa ikizingatiwa kwamba viazi hivyo vinatengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo vitafunwa. Amewashauri kuzingatia suala la usindikaji wa mazao yao ili kuvutia zaidi soko la ndani na nje ya nchi.

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana,  Kombe Danty, akizungumza kwenye uzinduzi wa Unga wa Viazi Lishe mkoani Mwanza.

Pudentia Ngereza ambaye ni Mwenyekiti wa Shirika la Sauti ya Mwanamke kutoka Ukerewe (Pia diwani Viti Maalumu Ukerewe), akizungumza wakati wa uzinduzi wa unga wa viazi lishe unaozalishwa na shirika hilo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora nchini ADLG, Jimmy Luhende, akizungumzia ubora wa matumizi ya viazi lishe wakati akinunua unga wa viazi hivyo baada ya kuzinduliwa rasmi hii leo mkoani Mwanza.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ) yenye makazi yake Jijini Mwanza, Deborah Mallaba, akitoa maelekezo kwa mgeni rasmi kuhusiana na mbogamboga na matunda zinazozaliwa na taasisi yake.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ) yenye makazi yake Jijini Mwanza, Deborah Mallaba,  akonesha bidhaa zinazozalishwa na taasisi hiyo ambapo mteja hujipatia hoho, nyanya, pilipili, chainizi, kabichi, karoti, bamia, mchicha, vitunguu, tangawizi, mchaichai, karanga, kisamvu, sukuma wiki, vitunguu swaumu, nyanya chungu na majani ya kunde ambapo kwa pamoja huuzwa kwa bei nafuu.

Aneth Shosha ambaye ni Mratibu/Masoko wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ), akonesha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na taasisi hiyo ambayo pia imekuwa ikiwaunganisha wakulima na wataalamu wa kilimo kupitia vyombo vya habari.

Simon Nkwabe Ng'wanakilala ambaye ni msaidizi katika Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ), akonesha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na taasisi hiyo ambayo pia imekuwa ikiwaunganisha wakulima na wataalamu wa kilimo kupitia vyombo vya habari.

Mgeni Rasmi amepokea zawadi ya vitafunwa zilivyotengezwa na Unga wa Viazi Lishe kutoka Shirika la Sauti ya Wanawake kutoka Ukerewe mkoani Mwanza.

Mgeni rasmi akiwa pamoja na wageni kutoka taasisi na mashirika mbalimbali kwenye picha ya pamoja.
Bonyeza HAPA Kusikiliza. Ama Bonyeza hapo chini.

0 maoni:

Chapisha Maoni