Posted by Esta Malibiche ob Dec30,2016 in NEWS
wanakijiji
cha Kitoga wakisikiliza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima
na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza katika mkutano wa
kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata
ya Vigwaza
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza kwa wananchi katika
mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha
Kitoga kata ya Vigwaza
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa maelekezo kwa
wanakijiji baada ya kufika katika kijiji cha Kitonga kutatua migogoro ya
wakulima na wafugaji.
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa
katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji
cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akisalimiana na watendaji mkoa wa Pwani
baada ya mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika
kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Kutokana
na kuendelea kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafugaji hapa nchini
,mbunge wa chalinze Mh RIDHIWANI KIKWETE ameiomba serikali kuchukua
hatua stahiki ili kulinda raia wake dhidi ya migogoro hiyo.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kitonga kata ya
Vigwaza mbele ya Mkuu wa Mkoa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Ridhiwani
amesema katika kijiji hicho kuna wafugaji ambao wameingiza mifugo
kwenye ranchi pamoja na kijijini pasipo kufata taratibu za
kisheria,jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wakulima wa kitonga,hivyo
ni vema serikali ikachukua hatua stahiki juu ya jambo hilo.
kama
ilivyoandikwa kwenye vitabu vya dini kuwa ombeni nanyi mtapewa,kilio cha
mbunge ridhiwani kikapokewa vyema na mkuu wa mkoa Mhandisi Ndikilo kwa
kutoa siku 30 ,kwa wafugaji waliovamia maeneo ya wakulima kuondoa mifugo
yao haraka iwezakanavyo,"Mlipokuja hamkugonga hodi hvyo na mnapoondoka
msituulize mtaenda wapi,haiwezekani ufugaji wako mtu mmoja uwe kero kwa
jamii inayokuzunguka hii si sawa"...alisema Ndikilo
RC
Ndikilo katika hatua nyingine ameagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha
wafugaji wote waliongiza mifugo hiyo kuondoka haraka iwezekanavyo, licha
ya wafugaji katika kijiji cha kitonga kudai kuwa wana ngombe wapatao
laki 5,lakini ukweli unaonesha kuwa kuna zaidi ya kiasi hicho,huku
akimtaka mmoja wafugaji anayeonekana kuwa mbabe kijiji hapo
aliyefahamika kwa jina moja la leki kuhakikisha anatii agizo la kuondoka
ndani ya mwezi mmoja haraka iwezekanavyo.
akionekana
kuchukizwa zaidi na vitendo vya wafugaji kuwanyanyasa wakulima ndikilo
amesema ni vyema wafugaji wakaelewa kuwa kila mmoja ana wajibu wa kutii
sheria ili watu waishi kwa amani na upendo.
kwaupande
wake mbunge wa chalizne mara baada ya kauli ya mkuu wa mkoa akawataka
wananchi wa chalinze kutoa ushirikiano kwa serikali ili kurahisisha
zoezi la kuondolewa kwa mifugo iliyoiungia kinyemela.
Wafugaji
wa kwanza kuingia mkoa wa pwani waliiongia mwaka 1940 ambao walikuwa
wamasai na tangu hapo ukawa mwanzo wa pwani kuwa na mifugo.
0 maoni:
Chapisha Maoni