Posted by Esta Malibiche on Dec 19,2016 in NEWS
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (Picha), leo tarehe 19 Desemba, 2016
amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 2 na Wakurugenzi 3 wa Mamlaka za Serikali za
Mitaa.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais
Magufuli amemteua Bw. Kisare M. Makori kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo katika
Mkoa wa Dar es Salaam.
Bw. Kisare M.
Makori anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Humphrey Polepole ambaye hivi
karibuni ameteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi
(NEC), Itikadi na Uenezi.
Halikadhalika,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Avod Mmanda Herman kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Mtwara iliyopo katika Mkoa wa Mtwara.
Bw. Avod Mmanda
Herman anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Khatib M. Kazungu ambaye hivi
karibuni ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Ramadhan Geodrey Mwangulumbi kuwa Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga iliyopo Mkoani Shinyanga.
Bw. Ramadhan Geodrey
Mwangulumbi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Lewis Kalinjuna ambaye
anastaafu kwa mujibu wa Sheria.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Bw Rojas John Romuli kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Mpanda iliyopo katika Mkoa wa Katavi.
Bw. Rojas John
Romuli anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ngalinda Hawamu Ahmada aliyefariki
dunia hivi karibuni.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Bw. Rashid K. Gembe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Mkinga iliyopo katika Mkoa wa Tanga.
Bw. Rashid K.
Gembe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Mkumbo Emmanuel Barnabas ambaye
uteuzi wake ulitenguliwa hivi karibuni.
Uteuzi wa huu
unaanza mara moja na wateule wote wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mara wapatapo taarifa
hii.
Gerson
Msigwa, Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
Salaam, 19 Desemba,
2016.
0 maoni:
Chapisha Maoni