Posted by Esta Malibiche on Dec 8,2016 in NEWS
Afisa
maendeleo ya jamii shirika la
kuhifadhi mazingira duniani [WWF-TANZANIA] Martha Sanga amewatka wananchi
kuhifadhi mazingira ili kuweza kujikinga na uharibifu wa Mazingira kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.
Akizngumza jana wananchi
wa mkoa wa Njombe wakati akifungua warsha
ya wadau mazingira iliyohusu kuhusu usimamizi wa wa rasilimali za maji
na mazingira iliyofanyika katika mji wa makambako mkoani Njombe.
Bi.Martha
alisema kuwa suala la usimamizi wa rasilimali za maji na mazingira sio la
wafadhili, bali ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha mazingira yanatunzwa.
‘’’
Ninawaomba wananchi na wadau mbalimbali wa mazingira wanabudi kuendelea hata
baada ya programu ya maji Ruaha kumaliza muda wake, kwani utunzaji wa mazingira
ni jukumu la kila mtu.Pia bado mapambano
ya utunzaji wa rasilimali za maji na mazingira yanaendelea
hata bila kuwepo wafadhili’’alisema Martha.
Alisema kuwa Shirika la WWF kwa kupitia Programu yake ya
Maji Ruaha (RWP) kwa kushirikiana na Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB),
halmashauri, wananchi na wadau mbalimbali wa mazingira walitekeleza mradi kwa
miaka mitano wa katika usimamizi wa rasilimali za maji na mazingira ambao
ulikuwa na lengo la rudisha hali ya Mto Ruaha Mkuu ili uweze kutiririsha maji
kwa mwaka mzima.
Evergris
Makfura nae ni Ofisa Maendeleo ya jamii ya jamii kutoka Shirika la WWF Tanzania kupitia Programu
yake ya Maji Ruaha alitoa rai kwa wadau kuendelea kuhifadhi mazingira na vyanzo
vya maji kwa kutumia dhana ya ushirikishwaji.
Makfura
lisema kuwa Serikali ilishaweka sawa mahitaji ya kisheria (legal framework)
kama vile kupitishwa kwa Sheria Mama ya Mazingira (2004), kutolewa kwa Sera ya
Maji (Julai 2002) na Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Namba 11 ya
mwaka 2009.
Alisema
lengo la Warsha hiyo ni kutathmini shughuli zilizotekelezwa na wadau mbalimbali
wa mazingira kwa kipindi cha miaka mitano cha utekelezaji ulioratibiwa na
shirika la WWF kupitia Programu yake ya Maji Ruaha kwa kushirikiana na Bodi ya
Maji Bonde la Rufiji (RBWB).
Kwa
upande wake Mhasibu wa Jumuiya ya Watumiaji Maji (WUA) katika Bonde dogo la Mto
Mpando wilayani Wanging’ombe, mkoani Njombe, Roy Kadege alisema kuwa jumuiya
hiyo atahakikisha inasimamia kikamilifu suala zima la usimamizi wa rasilimali
za maji na mazingira.
Kadege
alisema kuwa pamoja kuwa mradi
kumaliza muda wake, wataendelea kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa vile
vyanzo vingi vya maji vipo katika ukanda wao na ambako vyanzo vya mito
vinakoanzia.Alisema kuwa kupitia programu ya Maji Ruaha, jumuiya hiyo ya
watumiaji wa maji imeweza kutoa elimu ya usimamizi wa rasilimali za maji na
mazingira katika vijiji 20 vinavyozunguka bonde dogo la Mto Mpando.
Alisema kuwa baada ya kuwepo mradi huo wameweza kutunza
vyanzo vya maji na kupelekea kurudisha Mto Mbarali mkoani Mbeya ambao hapo
awali Mto huo ulikauka kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi zisizo
endelevu,lakini lakini kutokana na uwepo wa mradi huo mto umeweza kurudi katika
hali yake na kutunza mazingira
Mwenyekiti wa jumuiya ya watumia maji (WUA)
katika bonde la mto Mpando Adamson Msigala alisema kuwa, ili zoezi la usimamizi
wa rasilimali za maji na mazingira liiweze kuwa endelevu kila halmashauri zinatakiwa kutenga fedha kwenye bajeti zao kwa ajili ya
shughuli za utunzaji mazingira kuliko kutegemea wafadhili.
Msigala
alisema kigezo cha umaskini kisiwe chanzo cha kuharibu mazingira ni lazima watu
wafanya kazi kutunza mazingira bila kusukumwa bali kwa moyo.Wakati WWF wanaleta
mradi huo kwa mara ya kwanza, wananchi walikuwa wagumu kuuelewa kwa vile
walikuwa wamezoea kulima kwenye vinyungu ambavyoviko karibu na vyanzo vya maji.
“Kwa
kuwa wadau wetu wa maendeleo wanamaliza mradi wao haina maana kwamba shughuli
za usimamizi wa rasilimali za maji na mazingira zatasimama rahasha, sasa ni
jukumu letu wananchi kwa shirikiana na halmashauri zetu kuweka mikakati
yakuweza kuendelea pale wadau wetu walipoishia,” alisema Msigala.
Ofisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Wanging’ombe, mkoani
Njombe Michael Haule ambaye pia ni timu ya wawezeshaji ya wilaya (DFT)
alilipongeza shirika la WWF kupitia programu ya maji Ruaha pamoja na Bodi ya
Maji Bonde la Rufiji (RBWB) kwa kuwaunganisha wadau mbalimbali wa mazingira ili
kuweza kupanga mipango yao kwa pamoja.
Haule
alisema kuwa siku nyingine za kunapokuwa na warsha kama hizo washirikishe na
vyombo vya usalama na mahakama ili waweze kutambua jumuiya za watumia maji kuwa
zipo kisheria.
Bila kushirikisha vyombo hivyo usimamizi wa rasilimali za
maji na mazingira utakuwa mgumu kwa vile kutakuwa na na mwingiliano wa shughuli
baina ya vyombo hivyo na jumuiya za watumia maji. Kuna wakati fulani jumuiya za
watumia maji zilikuwa zikiwakamata waharifu wa uharibifu wa vyanzo vya maji na
wakipelekwa polisi wanatolewa,Kumbe kungekuwa na ushirikishaji wa vyombo hivyo
na vikatambua kuwa jumuiya za watumia maji zipo kisheria wangeweza kwenda
pamoja.’’’’alisema Haule
Hata
hivyo aliongeza kuwa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji
wanapoitisha mikutano yao wahakikishe wanawaalika taasisi ya kupambana na
rushwa (TAKUKURU), polisi na mahakama ili waweze kuvitambua vyombo hivyo vya
watumia maji ili kusimamia kikamilifu suala zima la rasilimali za maji na
mazingira.
0 maoni:
Chapisha Maoni