Posted by Esta Malibiche on Dec 8,2016 in MICHEZO
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wachezaji wa Timu ya
Mpira wa Miguu, Miembeni Club kabla ya timu hiyo kupambana na Timu ya
Taifa Jang’ombe katika Uwanja wa Amani, Zanzibar. Masauni aliwaambia
wachezaji wa Timu hiyo inayotoka katika Jimbo lake, wajitume na
wahakikishe ushinde unapatikana. Hata hivyo timu hizo zilitoka sare kwa
kufungana goli moja kwa moja.Picha na MOHA.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa kofia) akiwa na
Katibu wa Timu ya Miembeni, Simai Mwalimu wakiingia ndani ya Uwanja wa
Amani, Zanzibar kwa ajili ya kushuhudia timu hiyo inayotoka katika Jimbo
la Masauni, ikipambana na Timu ya Taifa Jang’ombe katika mzunguko wa
Ligi Kuu visiwani humo.Picha na MOHA.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwa na Katibu wa Timu ya
Miembeni, Simai Mwalimu wakiangalia wachezaji wa Timu ya Miembeni
(hawapo pichani) ilipokuwa inafanya mashambulizi dhidi ya Timu ya Taifa
Jang’ombe katika mzunguko wa Ligi Kuu ya Zanzibar zinazofanyika katika
Uwanja wa Amani, mjini Unguja. Timu hizo zilitoka sare kwa kufungana
goli moja kwa moja. Picha na MOHA.
Mchezaji
wa Timu ya Miembeni akipiga mpira kichwa akimtoka mpinzani wake wa Timu
ya Taifa Jang’ombe katika mechi ya Ligi Kuu Zanzibar iliyofanyika
katika Uwanja wa Amani na Timu hizo zilitoka sare kwa kufungana goli
moja kwa moja. Picha na MOHA
Mashabiki
wa Timu ya Miembeni wakishangilia wakati timu yao ilipokuwa imeifunga
goli moja, Timu ya Taifa Jang’ombe, katika mashindano yaliyofanyika
katika Uwanja wa Amani, Zanzibar.Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni
(hayupo pichani) alihudhuria timu hizo zikipambana katika mzunguko wa
Liki Kuu visiwani humo.Picha na MOHA.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kofia) akiwa katika picha ya
pamoja na wachezaji wa Timu inayocheza Ligi Kuu, Miembeni Club pamoja
na viongozi wao kabla ya timu hiyo kuanza kucheza na Timu ya Taifa
Jang’ombe. Timu hiyo inatoka katika Jimbo la Masauni, ambapo aliwasili
uwanjani hapo kwa lengo la kuwahamasisha wachezaji hao watoke na
ushindi. Picha zote na MOHA.
0 maoni:
Chapisha Maoni