Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Ijumaa, 30 Desemba 2016

MBUNGE WA JIMBO LA KILOLO MWAMOTO ,ACHANGIA MILIONI 6 KUKARABATI SHULE


Posted by Esta Malibiche on Dec 30,2016 in NEWS
Mbunge  wa  Kilolo Venance  Mwamoto (wa  pili kulia)  akitoka kukagua  shule  ya Msingi Mazombe  ambayo ni  shule  aliyosoma  aliyekuwa  mbungbe  wa  jimbo la  Kilolo Prof Peter Msola na kuahidi  kuikarabati  upya  shule   hiyo  kutokana na uchakavu iliyonao
Hili  ndilo  jengo  lenye  mwonekano mzuri Mazombe shule ya Msingi
Mtendaji wa kijiji  cha Ikula Patricia Nyomolelo  akimsikiliza mbunge Mwamoto
Familia ya mwalimu  wa  shule ya Msingi Ikula  ikiwa  nje ya  nyumba yao
Mbunge  wa  Kilolo Venance  Mwamoto  akiwa ameshika kiuno baada ya  kuonyeshwa  nyumba  anayoishi mwalimu mkuu wa  shule ya msingi Ikula  wilaya ya  Kilolo ambayo  madirisha  yake  yamewekwa mabati na  kuahidi kuziboresha  nyumba   hizo jana  wakati wa ziara  yake ya  kukagua miradi ya maendeleo katika  shule   hiyo
Mbunge  Mwamoto  akisalimiana na walimu wa Ikula  waliokuwa ndani ya  nyumba  yao
Mbunge  Mwamoto wa tatu  kulia  akitazama mchezo kati ya  Simba na Ruvu pamoja na  wapiga kura wake
Mwalimu  wa shule ya Msingi Ikula akiwa na mbunge Mwamoto 
Na MatukiodaimaBlog 
MBUNGE  wa  Kilolo mkoani  Iringa amechangia kiasi cha Tsh  milioni 1 kwa  ajili ya  ukarabati  wa  shule  ya  Msingi Mazombe ambayo   viongozi mbali  mbali  wamesoma katika  shule   hiyo akiwemo aliyekuwa  mbunge wa   jimbo hilo kabla yake Prof Peter Msolla  huku kiasi cha Tsh  milioni milioni 7  zikitolewa kwa  shule ya Kiheka  sekondari  na shule ya msingi Ikuvala kwenye kata ya  Nyalumbu  inayoongozwa na  diwani wa chama  cha  Demokrasia na maendeleo (chadema)

Mwamoto  ambaye  katika ziara  yake  ya ukaguzi wa  miradi ya maendeleo  inayoendelea  katika  jimbo  hilo la  Kilolo ametumia  kiasi cha  Tsh milioni 45  za  mfuko  wa  jimbo  kuunga mkono  jitihada mbali  mbali za  wananchi wake  alisema kuwa  huu si  wakati wa siasa ni  wakati wa  kuwatumikia wananchi wote  bila  kuwabagua kwa itikadi za  kisiasa .

Akizungumza na  uongozi wa shule ya Msingi Mazombe jana  baada ya  kufanya ziara ya ghafla shuleni hapo  kukagua  shule   hiyo alisema haitapendeza   kuona anaitelekeza shule   hiyo ambayo  ni  shule  aliyosoma mtangulizi wake katika  ubunge Prof Msolla hivyo  kuahidi kuikarabati vizuri  na  kuwa  shule  yenye ubora  kama  shule  nyingine .

“Natambua  mchango  wa Prof  Msolla katika wilaya ya  Kilolo na Taifa   itakuwa  si busara  kwangu kama mbunge  kushindwa  kuikarabati  shule  hii ya Mazombe …..naomba  ukarabati  uanze  mara  moja kwa  kuweka  madirisha  na  sakafu nzuri  nje  ya hii ambayo ni mashimo mashimo” alisema  mbunge  huyo

Kuwa  kwa  ajili ya kuonyesha kuwa  huu ni  wakati wa kazi kwa kila  kiongozi  kuwatumikia  wananchi  bila  kuwabagua kwa itikadi  zao amefika katika ya  Nyalumbu  ambayo ni moja kati ya kata  mbili  za  wilaya ya Kilolo zinazoongozwa na  madiwani wa  Chadema  na  kuchangia  miradi ya maendeleo inayoendelea katika kata   hiyo .

Hivyo  aliwataka  wananchi  na  wanasiasa  katika  wilaya ya  Kilolo kwa  sasa  kuungana pamoja  kuleta maendeleo  kwani  huu si wakati wa siasa  ni wakati wa  wanasiasa  kuwatumikia wananchi  wao kwa  vitendo  si maneno  .

Katika  shule ya msingi Ikula  mbunge  huyo amechangia Tsh  milioni 1 ili  kukamilisha  ujenzi  wa  vyoo vya  wanafunzi shuleni hapo huku  akieleza  kusikitishwa na mvutano wa madaraka katika  kijiji   hicho   na kupelekea  wananchi  kushindwa  kuendelea na ujenzi wa nyumba ya  mwalimu  kwa  zaidi ya miaka  miwili  sasa  nyumba  kutokamilika .

Hivyo  alisema atamjulisha mkuu  wa  wilaya na  mkurugenzi ili  kufika  kutatua mgogoro  huo na  kuona namna gani Halmashauri  inaweza  kuunga mkono  jitihada za  wananchi hao hasa  kumalizia nyumba hiyo na wodi ya  wazazi japo kwa  upande  wake  ameahidi  kutoa bati za  kuezekea nyumba  hiyo ya  mwalimu  itakapomalizika.
 
Mwakilishi  wa  mkurugenzi  mtendaji  wa Halmashauri ya  Kilolo Henry Kaywanga  alisema kuwa  Halmashauri  ya  Kilolo  imechangia miradi mbali  mbali ya maendeleo ya  wananchi  kiasi cha Tsh milioni 120 zilizotumwa kama  ruzuku ya  serikali  (LGDG-CDG) .
Alisema  baadhi ya maeneo  miradi imekuwa  ikisuasua  kutokana na migogoro  ya viongozi  na kuwa  jitihada za  kufika katika maeneo  hayo yenye  migogoro  zimekuwa  zikifanyika na katika  kijiji cha Ikula watafika  kushughulikia mgogoro huo.
 Image result for DC Kilolo
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah  akizungumza na  mwandishi  wa habari  hizi kwa  njia ya  simu  juu ya ombi la wananchi  wa  Ikula  kutaka  kufika  kumaliza tofauti zao  alisema  kuwa toka  ameteuliwa  kuwa  mkuu wa  wilaya ya  Kilolo na mheshimiwa Rais Dkt  John Magufuli amekuwa  hakai ofisini  kila siku ni kuzungukia wananchi vijijini na  kuwa  kijiji  hicho ni miongoni mwa  vijiji ambavyo vipo kwenye  ratiba  wakati  wowote  kuanzia sasa atafika .
 
Alisema  kuwa  kuna baadhi ya maeneo alifika  na kutoa maagizo ya  kukamilisha  miradi na  tayari miradi  husika  imekamilishwa  na kutolea  mfano  kijiji  cha Mahenge  wanafunzi wa  awali  shule ya msingi Mlowa  walikuwa  wakisomea chini ya mti na katika ziara yake  alitoa agizo la  kujenga vyumba  viwili  vya madarasa ndani ya mwezi mmoja na wananchi  wamekamilisha ujenzi huo ndani ya  wiki tatu pekee.

KILIO CHA MBUNGE RIDHIWANI CHASIKIKA, RC NDIKILO ATOA MWEZI MMOJA KWA WAFUGAJI

Posted by Esta Malibiche ob Dec30,2016 in NEWS
wanakijiji cha Kitoga wakisikiliza  katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid  Mwanga  akizungumza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid  Mwanga akizungumza kwa wananchi  katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza  
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa maelekezo kwa wanakijiji baada ya kufika katika kijiji cha Kitonga kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji.
 
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid  Mwanga akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
 
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akisalimiana na watendaji mkoa wa Pwani baada ya mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Kutokana na kuendelea kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafugaji hapa nchini ,mbunge wa chalinze Mh RIDHIWANI KIKWETE ameiomba serikali kuchukua hatua stahiki ili kulinda raia wake dhidi ya migogoro hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza mbele ya Mkuu wa Mkoa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Ridhiwani amesema katika kijiji hicho  kuna wafugaji ambao wameingiza mifugo kwenye ranchi pamoja na  kijijini pasipo kufata taratibu za kisheria,jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wakulima wa kitonga,hivyo ni vema serikali ikachukua hatua stahiki juu ya jambo hilo.

kama ilivyoandikwa kwenye vitabu vya dini kuwa ombeni nanyi mtapewa,kilio cha mbunge ridhiwani kikapokewa vyema na mkuu wa mkoa Mhandisi Ndikilo kwa kutoa siku 30 ,kwa wafugaji waliovamia maeneo ya wakulima kuondoa mifugo yao haraka iwezakanavyo,"Mlipokuja hamkugonga hodi hvyo na mnapoondoka msituulize mtaenda wapi,haiwezekani ufugaji wako mtu mmoja uwe kero kwa jamii inayokuzunguka hii si sawa"...alisema Ndikilo

RC Ndikilo katika hatua nyingine ameagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wafugaji wote waliongiza mifugo hiyo kuondoka haraka iwezekanavyo, licha ya wafugaji katika kijiji cha kitonga kudai kuwa wana ngombe wapatao laki 5,lakini ukweli unaonesha kuwa kuna zaidi ya kiasi hicho,huku akimtaka mmoja wafugaji anayeonekana kuwa mbabe kijiji hapo aliyefahamika kwa jina moja la leki kuhakikisha anatii agizo la kuondoka ndani ya mwezi mmoja haraka iwezekanavyo.

akionekana kuchukizwa zaidi na vitendo vya wafugaji kuwanyanyasa wakulima ndikilo amesema ni vyema wafugaji wakaelewa kuwa kila mmoja ana wajibu wa kutii sheria ili watu waishi kwa amani na upendo.

kwaupande wake mbunge wa chalizne mara baada ya kauli ya mkuu wa mkoa akawataka wananchi wa chalinze kutoa ushirikiano kwa serikali ili kurahisisha zoezi la kuondolewa kwa mifugo iliyoiungia kinyemela.

Wafugaji wa kwanza kuingia mkoa wa pwani waliiongia mwaka 1940 ambao walikuwa wamasai na   tangu hapo ukawa mwanzo wa pwani kuwa na mifugo.

CCM KASULU YATOA ADHABU KWA MBUNGE NA MADIWANI WAKE KWA TUHUMA ZA KUCHOCHEA MGOGORO WA KUMPINGA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA KASULU

Posted by Esta Malibiche on Dec 30,2016 in SIASA

Na Rhoda Ezekiel- Kigoma,

KAMATI ya usalama na maadili na kamati ya siasa ya Wilaya ya Kasulu imetoa adhabu kwa Mbunge wa Viti maalumu wa Mkoa wa kigoma,Josephin Ngezabuke na madiwani sita wa Halmashauri ya mji wa Kasulu kwa tuhuma za kuchochea mgogoro wa madiwani kumpinga Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu kwamba aondolewe hafai.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana katibu muenezi wa Wilaya ya Kasulu Masoud Kitowe alisema kumekuwa na mgogoro Mkubwa uliodumu kwa miezi mitano wa Baadhi ya madiwani wa Act na CCM waliomuandikia barua Mkurugenzi ya kudai Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kasulu aondolewe hafai na Chama Cha mapinduzi hakikupatiwa barua hiyo ambayo ingeweza kuwasaidia kujua chanzo cha tatizo nini.
Alisema katika mgogoro huo madiwani wa CCM walio shiriki ni watano na kati ya hao mmoja ambaye ni Seleman diwani wa kata ya Kumnyika amepewa adhabu ya kalipio ambayo ataitumikia kwa miezi 18 kwa kosa na kushiriki kuandika barua ya kumkataa mwenyekiti wa Halmashauri hiyo wakati jambo hilo bado halijajadiliwa katika Kikao cha Chama kwamujibu sisi kama chama tulipo pata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi tuliwaita madiwani walio husika na kupewa onyo.
Aidha kitowe alisema madiwani wanne waliojiorodhesha kwenye barua ya kushiriki kumpinga Mwenyekiti huyo kamati ya siasa pia imetoa adhabu ambayo kwa Mujibu wa Sheria za Chama cha mapinduzi hairuhusiwi kuitangaza hazarani nao watatumikia adhabu hiyo kwa miezi 12.
Alisema Madiwani hao walipo hojiwa walikili mgogoro huo una chochewa na baadhi ya watu ambao ni Diwani wa Kata ya Murusi Steward Zinduse ambae alikuwa akigombea nafasi ya Mwenyekiyi wa halmashauri akashindwa pamoja na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Kigoma Josephini Ngezabuke nao pia wamepewa adhabu ambayo hairuhusiwi kutangazwa kwa mujibu wa sheria na barua walishapewa zinazo elezea adhabu zao.
Hata hivyo Kitowe alitaja sababu zinazo pelekea Mbunge huyo kumkataa Mwenyekiti wa halmashuri ni kwamba aliwahi kumuomba meya wa kasulu ashiriki vikao vya halmashauri ya Mji wa Kasulu baada ya kukataliwa kwakuwa ni mjumbe wa Baraza la madiwani kakonko alijenga chuki na Mwenyekiti huyo ,jambo la pili alimuomba mea amuite Everina diwani wa viti maalumu kwa madai avuliwe madaraka ya udiwani viti maalumu kutokana na migogoro ya kifamilia kati yake na diwani huyo wa viti maalum.
"Kwa mbunge wetu huyu migogoro ni kawaida yake ukiona kasulu kuna migogoro ujue kuna watu wanaochochea, ikumbukweMwaka 2010 kamati ya Siasa ya Mkoa ilimpa azabu ya kalipio mbunge huyo kutokana na migogoro kwakuwa yeye anadai anawatu juu watatengua adhabu hiyo ndio maana anaendelea na migogoro hiyo inayo pelekea Halmashauri kushindwa kufanya Shughuri za maendeleo suala ambalo hatulifurahii sisi kama Chama.

Alisema Madiwana hao watano baada ya kupewa adhabu waliachana na mgogoro huo lakini mpaka sasa Mbunge huyo pamoja na Diwani wa Kata ya Murusi alie kosa nafasi hiyo bado wanaendeleza Mgogoro huo suala ambalo halina masilahi katika chama zaidi ya kudhohofisha halmashauri yetu ya Mji wa Kasulu.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalumu Josephin Ngeza buke alisema hawezi kwenda kwenye halmashauri ya kasulu kuingia kwenye kikao na kufanya vurugu kwakuwa sheria ninazifahamu ninauwezwa kufanya vurugu hata nikiwa nje siwezi kupiga kura sehemu mbili yeye ni Mjumbe wa Halmashauri ya kakonko anacho hitaji ni yeye kupewa heshima kama Mbunge wa Mkoa anapo fika katika Halmashauri ya Wilaya ya kasulu nikeshimike kama Mbunge.
" mimi sio kwamba simuhitaji Mweenyekiti sina shida na mwenyekiti wala kurudi kwenye Baraza la mji wa kasulu mimi nitabaki Kakonko lakini ninacho hitaji niheshima mimi kama mwenyekiti wa UWT na Mbunge wa Mkoa mzima,Siwezi kuleta malalamiko yangu kwamba mtu kanifanyia vurugu nyumbani kwangu nisisikilizwe na hata Zinduse mwenyewe amekwisha ridhika na Mwenyekiti",alisema Ngezabuke.

MGANGA WA TIBA ZA ASILI ATATUA CHANGAMOTO YA MAJI NJOMBE

Posted by Esta Malibiche on Dec 30,2016 in NEWS




MGANGA mkogwe wa tiba Ya asili wa wilayani Njombe mkoani Njombe, Dk Antony Mwandulami akionyesha chanzo cha maji alichokihifadhi na kukitumia kusambaza maji kwa wananchi wa  kijiji chake cha Itunduma, wilayani humo.






 MGANGA mkogwe wa tiba ya asili wa wilayani Njombe mkoani Njombe, Dk Antony Mwandulami akionyesha kituo cha kuchotea maji baada ya kuifadhi chanzo cha maji na kuamua   kuyasambaza maji hayo  kwa wananchi wa  kijiji chake cha Itunduma, wilayani humo.




Dk Antony Mwandulami ambae ni  Mganga  mkogwe wa tiba za asili wa wilayani Njombe mkoani Njombe  ametumia zaidi ya Sh Milioni 65 kumaliza tatizo  la  upatikanaji wa maji lilikuwa likiwakabili   wananchi wa  kijiji  cha Itunduma, wilayani humo.

Akizungumza na Mtandao huu wa Habari ulipomtembelea juzi  kijijini na kufanya mahojiano maalum kuhusu namna alivyopambana na hatimae  kufanikiwa kutatua changamoto hiyo ya maji alisema; akiwa mkazi  wa kijiji hicho aliguswa sana na tatizo la ukosefu wa maji na ndipo alipoamua kukifufua chanzo cha maji hicho kilichopo mita 200 kutoka brabara kuu ya Njombe Makambako.

Dkt.Mwandulami alisema chanzo hicho chenye chemichemi nyingi kilikauka kutokana na kukithiri kwa shughuli za kilimo, ufugaji na ukataji wa miti.

 “Nilianza kwa kutumia zaidi ya Sh Milioni 18 kukirudisha chanzo hicho katika hali yake ya kawaida na kwa kushirikiana na serikali ya kijiji tukakihifadhi na kukilinda hadi kikaleta mafanikio yote hayo,” alisema Mwandulami

 Alisema baada ya kuanza kutiririsha maji alilazimika kujenga bwawa pembeni yake, akapandikiza samaki wa aina mbalimbali na kujenga njia za maji za kisasa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
“Mbali na bwawa hilo kuwezesha usambazaji wa maji majumbani na mashambani lakini limetoa ajira inayowaongezea kipato vijana wanaojishughulisha na uvuvi.Alisema Mwandulami 

Aidha alivitaka vijiji vyenye changamoto ya maji viende kijijini hapo vikajifunze namna bora na rahisi ya kuhifadhi na kulinda vyanzo vya maji kwa manufaa yao na ya vizazi vijavyo akisema maji ni uhai na ni maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho,  Medson Nyagawa alisema kabla ya kushughulikia changamoto hiyo  wananchi wa kijiji hicho walikuwa wanatembea umbari mrefu  kutafuta maji.
 Nyagawa alisema kuwa baada ya tatizo hilo kuwasumbua kwa muda mrefu Dk Mwandulami aliamua kutumia fedha zake kuhifadhi na kuanza kukilinda chanzo cha maji cha Nyhengeza, alichimba bwawa katika chanzo hicho, alipeleka umeme na pampu ya kusukuma maji na akajenga tenki lenye uwezo wa kuhifadhi lita 32,000 za maji.

 “Pamoja na kujenga tenki hilo akatengeneza mtandao wa kusambaza maji kwa wananchi na kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji,” alisema huku akimshukuru mganga huyo kwa mchango huo kwa jamii inayomzunguka’’.Alisema Nyagawa

 Mmoja wa vijana anayefanya shughuli ya uvuzi katika bwawa hilo, Samsoni Mwinami alimshukuru Dk Mwandulami akisema mchango wake huo, umemuhakikishia kupata wastani wa Sh 10,000 kila siku kutoka katika shughuli yake yake ya uvuvi katika bwawa hilo.