Posted by Esta Malibiche on Oct 25,2017 IN NEWS
Mgeni
rasmi ambaye ni afisa elimu manispaa ya Iringa MWL .Tupe Kayinga
akizungumza na walimu wanawake waliojitokeza kuelekea mkutano mkuu wa
chama cha walimu manispaa ya Iringa.
katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale akizungumza na walimu wanawake waliojitokeza kuelekea mkutano mkuu wa chama cha walimu manispaa ya Iringa.
Baadhi ya walimu wanawake waliohudhuria mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.
Walimu
wanawake manispaa ya Iringa walalamikia kutokuwepo kwa uwiano wa
viongozi wanawake na wanaume katika sekta nyeti kama vile wakuu wa
shule,maafisa elimu kata na wilaya wakati walimu wa wanawake ndio wengi
hivyo inafifisha ndoto za kuwa viongozi kwa kuwa wanauwezo wa kuongoza
na kusimamia mambo mengi yakaenda kama yalivyopangwa.
Hayo
yamesemwa na walimu wanawake katika mkutano mkuu wa chama cha walimu
wanawake kilichokuwa kinaongozwa na katibu wa wilaya mwl. Fortunata
Njalale katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.
Akisoma
risala iliyoandaliwa na kamati ya kitengo cha walimu wanawake MWL. Evon
Mhewa alisema kuwa walimu wanawake wamekuwa wakikumbana na changamoto
nyingi katika kukamilisha majukumu yao.
“Mwalimu
wa kike anacheleweshewa kulipwa madeni mbalimbali anayokuwa anaidai
serikali maana bila kulipwa madeni yetu walimu hawawezi kufundisha kwa
moyo kwa kuwa maisha yanakuwa magumu na kuwapelekea kubuni njia mbadala
za kujiingizia kipato” alisema Mhewa
Mhewa
alizitaja changamoto nyingine ni kutopata nyongeza ya mishahara ya kila
mwaka na kusimama kwa mwaka wa pili sasa,walimu kutopandishwa madaraja
na wengine kupandishwa na kupokwa mshahara pamoja na walimu wanawake
kutokuwa na uwiano wa vyote katika sekta nyeti.
“Sisi
walimu wa kike kwa sasa tumesoma sana na tunaweza kuwa viongozi sehemu
yoyote kwa kuwa tayari tumethibisha hilo kwa wanawake waliopewa kazi
hiyo kwani wameifanya ipavyo na kuleta matokeo chanya kwa serikali hivyo
tunaomba walimu wanawake tupewa nafasi katika ngazi ambazo tunastahili”
alisema Mhewa.
Akijibu
risala hiyo mgeni rasmi ambaye ni afisa elimu manispaa ya Iringa MWL
.Tupe Kayinga alisema kuwa ni kweli walimu wanamadi mengi serikalini
lakini akasema kuwa hiyo yote imetokana na swala la uhakiki wa watumishi
hivyo mchakato wa uhakiki ukimalizika kila kitu kitakuwa sawa
ninauhakika na hilo.
“Unajua
serikali imechelewesha maswala mbalimbali ambayo ni kero kwa walimu
kutokana na uhakiki hivyo nawaomba walimu wawe na uvumilivu kwa kuwa
kila kitu kitakuja kutengemaa kama ilivyokuwa hapo awali” alisema
Kayinga
Kayinga
aliwataka walimu wanawake kuendelea kusoma ili kuwa na elimu ndio
itakayowapa nafasi mbalimbali ambazo zinashikiriwa na walimu wanaume
hivyo bila kuwa na elimu walimu wanawake wataendelea kuongozwa na walimu
wanaume kila sekta.
“Najua
kuwa walimu wanawake wanakipawa cha kuwa viongozi lakini mitaala mingi
inataka walimu kuwa na elimu ili kupata kuongoza sekta mbalimbali sasa
inatubidi walimu kujiendeleza kimasomo ili kukidhivigezo ambavyo mara
nyingi imekuwa ni elimu ya walimu anayepaswa kupewa kitendo husika”
alisema Kayinga
Aidha
Kainga aliwataka walimu wanawake kugombea nafasi mbalimbali
zinazojitokeza ili kupata nafasi za kuongoza na sio kila wakati kuwaacha
walimu wanaume wakigombea pekee yao.
“Tumieni
fursa za kugombea nafasi zinazojitokeza msiogope wanawake mnatakiwa
kuwa mstari wa mbele kuogmbea kwa kuwa katika kada ya ualimu walimu
wanawake tupo wengi hivyo kuanzia saizi walimu wanawake amkeni mjitume
kuhakikisha mnagombea” alisema Kayinga
Naye
katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale
alisema kuwa mkutano huo ni wa kikatiba kwa mjibu wa katiba ya chama cha
walimu taifa hivyo katiba imewaagiza kukaa na viongozi wa walimu
wanawake kuzijadili changamoto za wanawake ili kuzipeleka katika mkutano
mkuu wa wilaya.
“Leo
tupo walimu wanawake pekee yetu ili kubaini changamoto zetu na
kuzipeleka kwenye mkutano mkuu na kuweza kuzitetea kwa pamoja ili
kuboresha maslai ya walimu wanawake ambao wamekuwa wanakumbana na
changamoto nyingi sana wawapo kazini” alisema Njalale
Njalale
alisema kuwa walimu wanawake wamekuwa na mwamko wa kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi kuwa wanauwezo wa kuwa viongozi na kuongoza kwa
kupata matokeo chanya.
“Tunakitengo
cha walimu wanawake taifa kimetusaidia sana walimu wanawake kupata
ujalisi na kuacha uoga kugombea nafasi mbalimbali hivyo kwa sasa walimu
wakiume wajipange sana maana walimu wanawake tumedhamilia kugombea
nafasi yeyeto itakayojitokeza katika chama chetu cha walimu” alisema
Njalale
Njalale
aliwapongeza walimu wanawake wanaothubutu kugombea nafasi mbalimbali
kwa kuwa wamekuwa wakishinda na wanafanya kazi ipasavyo na kusema kuwa
walimu wanawake wanaweza bila kuwezeshwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni