Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Anthoyn Mavunde akizungumza na waumini wa dini ya Kiislam mara baada ya dua maalum iliyosomwa leo hii katika Madrasa ya Darual Mustafa_Chang'ombe Dodoma Mjini.PICHA NA OFISI YA MBUNGE
Viongozi mbalimbali na waamini wa dini ya Kiislamu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Ndg Anthony Mavunde kwa utendaji kazi wake wa kuleta maendeleo katika Jimbo la Dodoma Mjini.
Pongezi hizo zimetolewa mapema leo hii wakati akisomewa Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Mjini Dodoma.
Viongozi hao wamempongeza Mbunge Mavunde kwa kugawa vitabu vya Misahafu 50,Juzuu 400 na Kanzu 300 katika misikiti mbalimbali iliyopo Dodoma Mjini.
Wamempongeza pia kwa kusimamia mabadiliko makubwa katika sekta za AFYA,ELIMU,MIUNDOMBINU,MICHEZO na UWEZESHWAJI WANANCHI.
Akitoa maelezo ya awali,Mwalimu wa Madrasa Ustadhi Omar Salum Itara amemshukuru Mavunde kwa msaada mkubwa alioutoa katika Madrasa hiyo ikiwa pamoja na kuwawekea umeme ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea kujifunza mpaka usiku.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Anthony Mavunde,akizungumza katika Dua hiyo, aliwashukuru Viongozi na waamini wa dini ya kiislamu kwa namna wanavyomuunga mkono katika shughuli mbalimbali za kuwaletea maendeleo na kuwaomba waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu atimize majukumu yake vyema.
Mavunde ametoa Msaada kwa Spika moja moja kwa Misikiti 16 zenye thamani ya Tsh 4,000,000 Pia ameahidi kukabidhi Laptop 2 zenye thamani ya Tsh 1,000,000 na milango miwili yenye thamani ya Tsh 500,000 kwa ajili ya madrasa ya Darul Mustafa.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni