Jumatatu, 23 Oktoba 2017

Waziri wa Maliasili Dk.Kigwangalla amefuta vibali vyote vya uwindaji kwa makampuni

Posted by Esta Malibiche,on Oct 23,2017

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla  amefuta vibali vyote vilivyotolewa na Wizara yake vya Uwindaji wa makampuni,kauli hiyo ameitoa Mkoani Dodoma wakati akizungumza na wadau wa Maliasili na Utalii.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla leo Oktoba 22,2017 amefuta vibali vyote vilivyotolewa na Wizara yake vya Uwindaji wa makampuni ilikuwa na utaratibu mpya wa uombaji kwa njia ya mnada.
Waziri Dk.Kigwangalla ametoa agizo hilo jioni hii wakati wa kuhitimisha mazungumzo yake na wadau mbalimbali wa sekta ya Utalii na Maliasili aliokutana nao mjini hapa Dododma.
“Kwa mamlaka niliyonayo. Natamka kwamba, nafuta rasmi vibali vyote vya Uwindaji kwa makampuni vilivyotolewa na wizara yangu kwa mwaka huu. Pia naagiza Watendaji wote wanaosimamia ili, wahakikishe wanaandaa mchakato ndani ya siku 60 ili mchakato huo wa mnada ufanyike na uwe wa uwazi” alieleza Dkt. Kigwangalla.
Pia ametoa onyo na maagizo mazito kuhakikisha kuwa vitalu vyote vyenye migogoro ikiwemo vile vya Loliondo, Natroni na maeneo mengine kutotolewa kwa vibali vya uwindaji mpaka hapo watakapokamilisha tatizo la migogoro hiyo.
Aidha, ametoa agizo kwa hoteli 10 zilizobinafsishwa kutoka Serikalini zirejeshwe ndani ya siku 60 kuanzia sasa huku akiagiza watendaji waandike barua kwa msimamizi wa hazina

0 maoni:

Chapisha Maoni