Posted by Esta Malibiche on Oct 25,2017 IN NEWS.
Katibu
tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka akiwa kwenye mkutano mkuu
wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa akizungumza
na baadhi ya walimu walihudhuria mkutano huo.
Baadhi ya walimu waliokuwa wanaimba wimbo wa walimu wakati wa mkutano
mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa
uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.
Walimu
wa halmashauri ya manispaa ya Iringa wametakiwa kutumia kondomu ili
kujikinga na magonjwa ya zinaa amboya yamekuwa yakipunguza nguvu kazi ya
taifa.
Hayo
yamesemwa na katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka wakati
wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa Mjini,mkoani hapa.
Chintinka
alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la waathirika wa ugonjwa wa ukimwai
kutokana na kufanya mapenzi bila kutumia kondomu.
“Jamani
hapa Iringa kuna tatizo kubwa la ugonjwa wa ukimwi hivyo niwaombe
walimu wangu tutumie kondomu ili kujiepusha na gonjwa hili vinginevyo
vizazi vyetu vyote vitaambukizwa ukimwi” alisema Chintinka
Chintinka
alisema njia ya kuwa salaama kuepukana na gonjwa hili ni kujikinga kwa
kutumia kondomu maana hata watoto wetu wameathirika kutokana na wazazi
kutokuwa makini na matumizi ya kinga
“Naombeni
tuwakinge hawa watoto wetu ambao wameathirika ili wasiwaambukize watoto
wengine maana bila hivyo tutakuwa na kizazi kilichoathirika” alisema
Chintinka
Aidha
Chintinka aliwaomba walimu walioathirika kujitokeza ili kupewa lishe
ambayo inatolewa na serikali bure hivyo walimu wametakiwa kujitokeza na
kuweka wazi kwa mwagili wake ili aweze kupata mgao wa pesa za lishe.
“Jamani
walimu fungu la lishe kwa walimu walioathirikia ni nono kweli naombeni
walimu mjitokeze ili mfaidi fungu hili nono maana mimi nafahamu sisi
ndio tunaotenga naombeni fikisheni ujumbe huu kwa walimu wengine ambao
hawajafika hapa” alisema Chintinka
Chintinka
aliwataka watumishi wanaotoa siri za watumishi walioathirika kuacha
tabia hiyo mara moja ili kuwaweka huru waathirika na wengine waweze
kujitokeza na wapate lishe iliyotengwa na wilaya.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa chama hicho manispaa ya Iringa MWL. Zawadi
Mgongolwa alikiri kuwepo kwa viongozi wa sekta hiyo ambao wemekuwa
wakitoa siri za walimu na watumishi walioathirika na ugonjwa wa ukimwi.
Kwa
kweli mgeni rasmi umeongea ukweli kero kubwa kwa walimu ni kutolea siri
nje kitu kinachowafanya walimu waathirika kujificha na maradhi yao”
alisema Mgongolwa
Naye
katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale
alimpongeza mgeni rasmi kwa ujumbe wake ambao umekuwa faraja kwa walimu
na kuwaongezea hali ya kwenda kufanya kazi ya uwalimu kwa kujituma na
kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wao.
0 maoni:
Chapisha Maoni