Ijumaa, 27 Oktoba 2017

Bodi Ya Filamu Fanyeni uUtafiti Kuona Takwimu Za Mapato Ya Sekta Ya Filamu – Mhe. Shonza

Posted by Esta Malibiche on Oct 27,2017 IN NWS

Pix 2
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza na watendaji wa bodi ya filamu (hawapo pichani) wakati wa ziara yake kutembelea ofisi za Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam


Pix 1
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (kulia) akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) kutembelea ofisi za Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akiangalia vitambulisho kwa ajili ya wasambazaji wa filamu wa Barazani alipofanya ziara katika ofisi za Bodi ya Filamu na kutembelea wadau wa filamu Barazani jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Pix 4
Mkurugenzi wa Barazani Bw. John Kallaghe (kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) namna mwananchi anavyoweza kununua kopi ya filamu kupitia simu ya mkononi jana wakati wa ziara yake katika ofisi za Bodi ya Filamu na baadaye kutembelea wadau wa filamu wa Barazani Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Pix 5
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (watatu kulia) katika picha ya pamoja na viongozi wa shirikisho la filamu na wadau wa filamu kutoka Barazani baada ya kufanya ziara katika ofisi za Bodi ya Filamu na baadaye kutembelea wadau wa Barazani Jana Jijini Dar es Salaam. Wanne kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Pix 6
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akiweka sawa kipaza sauti alipotembelea Studio za Wanene Entertainment baada ya kufanya ziara katika ofisi za Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam
Pix 7
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (watatu kulia) akiangalia namna kazi za sanaa zinavyoandaliwa alipotembelea Studio za Wanene Entertainment baada ya kufanya ziara katika ofisi za Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Pix 8
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Studio za Wanene Entertainment Bw. Dash Pandit (katikati) alipotembelea Studio hizo baada ya kufanya ziara katika ofisi za Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
…………………
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Tarehe: 27/10/2017
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ameitaka Bodi ya Filamu Tanzania kufanya utafiti na kukusanya takwimu sahihi za mapato yatokanayo na sekta ya filamu nchini ili kuweza kubaini sekta hiyo inavochangia katika pato la taifa.
Hayo ameyasema jana Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika Ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania na kuzungumza na watendaji wa bodi hiyo huku akiwataka kuweka mifumo ambayo itasaidia wasanii kuinua, kuboresha na kuendeleza tasnia ya filamu nchini.
Aidha Mhe. Shonza ameitaka bodi ya filamu kuhakikisha kuwa inasimamia maadili katika filamu pamoja na ubora wa filamu ili filamu zinazotengenezwa inchini ziwe na kiwango kitakachowavutia wadau wa filamu ndani na nje ya nchi kupenda filamu zetu.
Mhe. Shonza amesema kuwa katika kukuza vipaji Bodi ya filamu ifanye jitihada za kuwafikia na kutoa elimu kwa wanatasnia ya filamu waliopo mikoani kwani huko nako kuna wasanii wenye uwezo wa hali ya juu lakini vipaji vyao havionekani kutokana na kutofikiwa  kwa wakati.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amemhakikishia Mhe. Naibu Waziri kuwa Bodi ya Filamu itaendelea kukaza kamba na kuhakikisha kuwa haioni haya katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu ya sheria na kanuni zilizopo.
Bibi. Fissoo amesema kuwa kati ya mwaka 2011 hadi sasa bodi ya filamu imesambaza jumla ya nakala elfu thelathini za sheria na kanuni katika Mikoa na Wilaya zote nchini ili shughuli za filamu zinazofanywa mikoani ziweze kuendana na sheria na kanuni zilizopo katika sekta ya filamu.
Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Simon Mwakifwamba amemshukuru Naibu Waziri Shonza kwa kuonyesha hari ya kuipigania sekta ya filamu mara tu baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri kwani kwa kufanya hivyo kunawapa moyo wanatasnia ya filamu kuelekea katika mapinduzi ya filamu nchini.

0 maoni:

Chapisha Maoni