Posted by Esta Malibiche on Oct 27,2017 IN NEWS
Katika awamu hii ya kwanza zaidi ya wazee 1,080 watapata Vitambulisho huku wazee 540 ndio wamekabidhiwa leo hii na wengine wataendelea kupokea kutoka katika Ofisi ya Mbunge kwa muda wa wiki nzima huku matarajio yakiwa ni kuwafikia wazee 3,284 katika jimbo zima.
Aidha; sherehe hizo zimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe. Godfrey Ngupula ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi.
Katika hotuba yake,alimpongeza bunge kwa jitihada zake za kuhakikisha wananchi wanaondokana na chanagamoto mablaiambali zilizokuwa zinawakabili,ikiwa nipamoja na kuwaletea maendeleo,kuwatumikia ikiwa ni mojanya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
"Jimbo la Nzega Mjini ni jimbo pekee ndani ya Halmashauri ya Mji wa Nzega hivyo tukio hili linaifanya Halmashauri hii kuwa moja kati ya Halmashauri chache kitaifa kutekeleza kwa vitendo Sera ya Taifa Matibabu ya Bure kwa wazee." Alisema Ngupula
Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini kupitia Chama cha Mapinfuzi CCM Hussein Bashe akiendelea kukabidhi vitambulisho vya matibabu ya bure kwa wazee wa jimbo la Nzega Mjini.PICHA NA OFISI YA MBUNGE. |
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe. Godfrey Ngupula ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi,akikabidhi vitambulisho vya matibabu kwa wazee wa jimbo la Nzega Mjini.PICHA NA OFISI YA MBUNGE. |
Wazee wa jimbo la Nzega Mjini wakiwa katika tukio la kukabidhiwa vitambulisho vya matibabu vilivyotolewa na mbunge wao Hussein Bashe.
0 maoni:
Chapisha Maoni