Ijumaa, 27 Oktoba 2017

MGOMBEA WA UDIWANI CCM KATA YA MBWENI WILAYANI KINONDONI AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA UDIWANI

Posted by Esta Malibiche on Oct 27,2017IN SIASA

Mgombea wa udiwani kata ya Mbweni Wilaya ya Kinondoni kupitia chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Mbonde akikabidhi fomu kwa Afisa Mtendaji wa kata hiyo Ndugu Ibrahimu.

Mgombea udiwani  kata ya Mbweni Wilaya ya Kinondoni,kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Ndugu Mbonde amerusha fomu katika ofisi za kata hiyo jana,huku akisidikizwa na Katibu mwenezi wa ccm wilaya ya Kinondoni Bi.Joha Dobe, kada wa chama cha Mapinduzi CCM ndugu Gaston Francis pamoja na Comrade Makoba
Fomu hiyo ilipokelewa  na Afisa mtendaji wa kata hiyo Ndugu Ibrahimu.
Uzinduzi wa kampeni za Ccm katika uchaguzi huo Mdogo wa udiwani zinatarajia kufanyika siku ya jumapili ya tarehe 29,10,2017.

Mgombea wa udiwani kata ya Mbweni akisaini Fomu katika ofisi ya kata hiyo tayari kuikabidhi.

Katibu wa Itikadi na uenezi ccm Wilaya ya Kinondoni Bi.Joha katikatati akiwa na Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM Gaston Francis kushoto pamoja na Comrade Makoba kulia.





0 maoni:

Chapisha Maoni