MZUNGUKO wa Ligi ya Kombe la SPANEST Okoa
Tembo Piga Vita Ujangili iliyozinduliwa Oktoba 21, mwaka huu katika uwanja wa
Kimande, Pawaga; unaendelea kesho Jumatano kwa michezo sita itakayopigwa katika
viwanja mbalimbali vya Tarafa ya Pawaga.
Katika mzunguko huo, washindi wa pili wa
kombe hilo mwaka 2016, Kinyika FC watakuwa
uwanja wa nyumbani wakiikaribisha Isele FC.
Katika kijiji cha Ilolompya, Ilolompya FC
itakuwa mwenyeji wa Magozi FC huku Mkombilenga FC ikiikaribisha katika uwanja
wake wa nyumbani Luganga FC.
Nayo Mbuyuni FC itakuwa mwenyeji wa
Kimande FC wakati Magombwe FC itaikaribisha Kisanga FC na Mboliboli FC
itaikaribisha Mbugani FC.
Ligi hiyo inayopigwa kwa mwaka wan ne sasa
inazishirikisha timu 24 za vijiji vya tarafa ya Idodi na Pawaga vinavyopakana
na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa upande wa wilaya ya Iringa.
Mratibu wa Spanest Godwell Ole
Maing’ataki amesema mshindi wa kwanza wa ligi hiyo inayopigwa kwa mwezi mmoja
ataondoka na kombe, medali za dhahabu, seti moja ya jezi, cheti, Sh Milioni
Moja taslimu na atapata fursa ya kutembelea hifadhi ya taifa ya Ruaha.
Wakati mshindi wa pili wa ligi hiyo
ataondoka na medali za shaba, cheti, mipira miwili na Sh 700,000 taslimu,
mshindi wa tatu ataondoka na cheti, medali na Sh 500,000.
0 maoni:
Chapisha Maoni