Mkuu wa wilaya ya mbulu Mkoani Arudha,Chelestino s Mofuga jana 26/10/2017 alikuwa mgeni rasmi katika shule ya msingi Dongobesh ambapo aliakwa kufuatia shule hiyo kufanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba mwaka 2017 kwa kutoa vijana kumi waliopata wastani A. Akizungumza na jumuiya ya shule hiyo amekemea vikali tabia ya wanaume wanowapa mimba wanafunzi na kukatisha ndoto zao.
Ndugu zangu,serikali aitamuonea aibu mtu yeyote anayekwamisha ndoto za watoto wa kike kwa kuwapa mimba,tutamchukulia hatua za kisheria""Alisema Mofuga Mofuga alirudia KAULI yake kwamba mwanaume yeyote anayeona anapata mhemko akiwaona watoto wa kike wamevaa sare za shule, basi anashauriwa kwenda kumshonea mwenza wake sare za shule ili kupunguza tamaa dhidi ya watoto wa shule. Kwani akipatikana serikali itachukua hatua za kumfunga miaka 30 bila huruma. Pia aliwataka wananchi wa mbulu kumuunga mkono Dkt John pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwani ni Rais wa ambaye amefanya kazi nyingi ambazo hazingeweza kufanywa hata kwa awamu nane, ni bora katika dunia kwa sasa kwa kupigania rasilimali za nchi na kuinua uchumi wa nchi na watu wake akiwajali wanyonge zaidi .
" Mh Rais ameandika historia ya dunia na anastahili kuandikwa katika rekodi ya dunia kuwa mwafrika na mtanzania wa kwanza aliyeweza kuwabana wazungu hadi kufikia makubaliano ya kugawana faida ya madini kwa asilimia 50, na kwamba fidia ya 700 bilioni zitalipwa kwa Tanzania."*Alisema Mofuga
Aidha aliwaomba wananchi wamuombee Rais wetu mpendwa kwa mungu kila siku ili adumu katika afya njema ili awahudumie watanzania kama alivyopanga na kadri mwenyezi mungu atakavyomuongoza. Pia amewaasa wazazi washirikiane na walimu katika kuwaleawatoto wao na sio kuwaachia walimu tu.
0 maoni:
Chapisha Maoni