posted by Esta Malibiche on Oct 25,2017 IN NEWS
Rai
hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Philip Isdor
Mpango (Mb) katika Mkutano na Sekta Binafsi nchini (TPSF), Jijini Dar es
Salaam.
Waziri
Mpango amesema kuwa ni vema Sekta Binafsi ikashirikiana na Sekta ya
Umma kwa kuwa zote zinategemeana na hakuna nchi iliyoendelea bila kuwa
na Sekta Binafsi ambayo ni imara.
“Sekta
Binafsi na Sekta ya Umma hazina budi kufanya kazi kwa kushirikiana kwa
karibu, tena kwa kuaminiana kwa faida ya Sekta zote mbili na kwa
maendeleo ya Taifa kwa ujumla” aliongeza Dkt. Mpango.
Amesema
kuwa, lengo la pande zote mbili ni kuharakisha utekelezaji wa azma ya
Serikali ya Awamu ya Tano ya kuongeza fursa za ajira, kipato cha
mwananchi na kuondokana na umasikini uliokithiri kwa kujenga Tanzania
inayoongozwa na uchumi wa Viwanda.
Dkt.
Mpango alifafanua kuwa Serikali imeendelea kuyafanyia kazi mapendekezo
mengi yaliyotolewa na Sekta Binafsi ikiwemo katika kuboresha mazingira
ya biashara nchini ikiwemo kuondoa baadhi ya kodi zilizokuwa kero kwa
wafanyabiashara.
Baadhi
ya hatua zilizochukuliwa ni pamoja na Serikali kufanya marekebisho
kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kumpa Waziri mwenye
dhamana ya masuala ya Fedha mamlaka ya kusamehe Kodi ya Ongezeko la
Thamani bila kuhusisha utaratibu wa kulipa kwanza Kodi ya Ongezeko la
Thamani na baadaye kuomba kurejeshewa (Refund) kwenye miradi
inayofadhiliwa na wadau wa maendeleo (Grants) au mikopo yenye masharti
nafuu (Concessional Loans) ambayo mikataba husika ina masharti ya kutoa
msamaha wa kodi hiyo.
“Hatua
hii itawezesha wakandarasi wanaotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo
nchini kutopata tena usumbufu katika kutekeleza miradi hiyo na miradi
kutekelezwa kwa muda uliopangwa” alisema Dkt. Mpango
Ili
kuvutia uwekezaji katika sekta za viwanda, kilimo cha mazao na mifugo
nchini, Serikali imesamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa za
mtaji (capital goods) za viwanda vya mafuta ya kula, nguo, ngozi, madawa
ya binadamu na mifugo ili kupunguza gharama za ununuzi/uagizaji wa
mashine na mitambo watakayonunua wawekezaji kwa ajili ya kusindika na
kutengeneza bidhaa mbalimbali.
“Serikali
sasa inatoza Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa kiwango cha asilimia
sifuri katika huduma zinazotolewa kwenye usafirishaji wa bidhaa/mizigo
nje ya nchi (ancillary transport services), hatua itayopunguza gharama
za usafirishaji katika bandari zetu na kuifanya Tanzania kuwa njia bora
zaidi ya kupitisha bidhaa zinazotoka nje ya nchi kwenda nchi nyingine
hususan zisizo na bandari.
Kwa
upande wa hali ya Uchumi, Waziri Mpango amesema kuwa robo ya kwanza ya
mwaka 2017, uchumi ulikua kwa asilimia 5.7, robo ya pili ulikua kwa
asilimia 7.8, hivyo kufanya nusu ya kwanza uchumi kukua kwa asilimia
6.8.
Baadhi
ya shughuli za kiuchumi zilizokuwa kwa kasi ni usafirishaji na uhifadhi
wa mizigo ambao umekua kwa asilimia 19.8, uchimbaji madini na mawe
asilimia 18.0, uzalishaji viwandani asilimia 9.3 na ujenzi asilimia 8.8.
Dkt.
Mpango alisema Sekta ya Benki kwa ujumla imeendelea kuwa imara ikiwa na
mitaji na ukwasi wa kutosha juu ya viwango vinavyokubalika kisheria.
Kwa kipindi cha mwaka 2009 hadi 2017 huduma jumuishi za fedha
zimeongezeka kutoka asilimia 15.8 hadi asilimia 65.3. Upatikanaji wa
huduma za kifedha umeongezeka kutoka asilimia 29 kwa mwaka 2009 hadi
asilimia 86 kwa mwaka 2017.
Aidha
kwa upande wa mikopo kwa Sekta Binafsi ilipungua kutokana na Benki
kuchukua tahadhari kutokana na kuongezeka kwa mikopo chechefu
(Non-performing loans) ambapo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilichukua
hatua kwa kupunguza kiwango cha amana ambacho benki za biashara
zinatakiwa kuhifadhi Benki Kuu kama dhamana kutoka asilimia 10 hadi
asilimia 8 na riba za mikopo ya benki hizo kushuka kutoka asilimia 16
hadi 12.
Naye
mwenyekiti mwenza wa Mkutano huo Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (Mb) amesema kuwa njia bora ya kutatua
matatizo ya Sekta Binafsi ni kuendelea kufanyika kwa majadiliano yenye
tija.
Mmoja
wa wajumbe wa Mkutano huo wa wafanyabiashara ambaye ni wakili wa
kujitegemea Bi. Eve Hawa Sinare amesema kuwa ni vema kuangalia mfumo
mzuri wa kuweka riba unaofanywa na Benki za biashara ili kuwa na uwiano
mzuri.
Vilevile
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Bw. Salum Shamte
ameishukuru Serikali kwa kuonesha nia ya dhati ya kushirikiana na Sekta
hiyo kwa lengo la kufanikisha ukuaji wa uchiumi wa Viwanda.
Waziri
mpango amewahakikishia wafanyabiashara kuwa Serikali itaendelea
kuhakikisha kuna majadiliano ya mara kwa mara na wadau hao ili kutatua
changamoto zao na pia ameahidi kuandaa Mkutano mwingine ambao utajikita
katika masuala ya kodi kabla ya Sekta Binafsi kuwasilisha mapendekezo ya
kodi.
Mkutano
huo wa Sekta Binafsi na Umma ni wa pili kufanyika, kwa mara ya kwanza
Mkutano kama huo ulifanyika tarehe 11 Aprili, 2017 mjini Dodoma ambapo
ulisaidia kutatua changamoto nyingi ikiwemo kusaidia kuongezeka kwa
ufanisi katika huduma za bandari nchini.
Imetolewa na:
Benny Mwaipaja
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Godfrey Simbeye akifafanua jambo
kwa wafanyabiashara waliohudhuria katika Mkutano kati yao na Serikali
uliolenga kujadili mafanikio na changamoto za pande hizo mbili,
uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
mweza wa mkutano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akielezea kuhusu umuhimu wa
majadiliano katika kutatua changamoto za kibiashara nchini, mkutano
uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza na
wafanyabiashara Jijini Dar es Salaam kuhusu umuhimu wa kupeleka taarifa
za changamoto zao Serikalini ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia)
akifuatilia majadiliano kati ya Sekta Binafsi na ya Umma yaliyofanyika
Jijini Dar es Salaam lengo likiwa kutatua changamoto mbalimbali.
Waziri
wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) na Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Walemavu, Mhe. Anthony
Mavunde (Mb) wakibadilishana mawazo wakati wa Mkutano kati ya Sekta ya
Umma na Binafsi.
Makamu
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Bw. Salum Shamte akishukuru
juhudi za Serikali katika kuzileta pamoja Sekta binafsi na ya umma,
wakati wa Mkutano kati ya Sekta hizo mbili Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akipeana
mkono na Mfanyabiashara Mohammed Dewji wakati wa Mkutano kati ya Sekta
Binafsi na Umma Jijini Dar es Salaam
Baadi
ya Wafanyabiashara Jijini Dar es Salaam wakifuatilia Mkutano kati ya
Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliolenga kutatua changamoto za Sekta
hizo ili kuharakisha ukuaji wa uchumi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa pili
kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Sera kutoka Wizara hiyo Bw. Shogholo Msangi na wafanyabiashara wakifuatilia maelezo kutoka kwa Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani)
kuhusu umuhimu wa majadiliano katika kujenga uchumi wenye tija kwa
Sekta Binafsi na ya Umma.
Waziri
wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani (Mb) akizungumza kuhusu namna
Serikali ilivyojipanga katika kutatua tatizo la Nishati ya umeme ili
kuweza kuchochea uchumi wa Viwanda wakati wa Mkutano kati ya Sekta
Binafsi na Umma uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni