Jumapili, 1 Oktoba 2017

MANISPAA YA KINONDONI YASAINI MIKATABA MIWILI YA UJENZI WA BARABARA CHINI YA MRADI WA UBORESHAJI WA JIJI LA DAR-ES-SALAAM (DMDP) YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILLINGI BILIONI 50.

Posted by Esta Malibiche on Oct.1,2017 IN NEWS

 Mstahiki Meya wa Manispaa Kinodoni Mhe. Benjamin Samwel Sitta akipokea mikataba iliyosaini ya ujenzi wa barabara chini ya mradi wa uboreshaji wa Jiji la Dar-Es-Salaam (DMDP) zenye thamani ya zaidi ya bil.50

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg. Aron Kagurumjuli, akisaini  mikataba miwili ya ujenzi wa barabara chini ya mradi wa uboreshaji wa Jiji la Dar-Es-Salaam (DMDP) zenye thamani ya zaidi ya bil.50
Mstahiki Meya wa Manispaa Kinodoni Mhe. Benjamin Samwel Sitta,akisaini  mikataba miwili ya ujenzi wa barabara chini ya mradi wa uboreshaji wa Jiji la Dar-Es-Salaam (DMDP) zenye thamani ya zaidi ya bil.50 

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg. Aron Kagurumjuli, amesaini mikataba miwili ya ujenzi wa barabara chini ya mradi wa uboreshaji wa Jiji la Dar-Es-Salaam (DMDP) zenye thamani ya zaidi ya bilioni hamsini 

Mikataba hiyo imesainiwa leo katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa uliopo Magomeni, na kuhudhuriwa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, wataalam wa ujenzi kutoka Manispaa, na wakandarasi waliopewa jukumu la ujenzi. Akizitaja Barabara hizo kuwa ni Barabara ya 

01. Makanya, 
02. Tandale Kisiwani, 
03. Kisukulu, 
04. Korogwe, 
05. External na 
06. Kilungule, 

ambazo zipo kwenye Awamu ya Pili na ya Tatu ya mradi, Mkurugenzi huyo wa Manispaa amesema zitajengwa kwa Kiwango cha Lami nzito, kitakachokidhi matakwa na mahitaji kwa ubora uliokusudiwa. 

Aidha amebainisha kampuni zitakazohusika na ujenzi wa barabara hizo kuwa ni kampuni ya China Civil Engineering Construction Operation, kutoka nchini China, na Kampuni ya hapa nyumbani ya Estim Construction Company Ltd, ambazo mbali na ujenzi wa kiwango cha lami, pia zitajenga 

01. Sehemu ya wapita kwa miguu, 
02. Mifereji ya maji ya Mvua, 
03. Madaraja, 
04. Calvart pamoja na 
05. Uwekaji wa taa na alama za Barabarani. 

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Benjamin Samwel Sitta, vamempongeza Mkurugenzi kwa kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha barabara za awamu ya kwanza ya mradi, zimejengwa kwa ubora uliokusidiwa. 

Aidha amewataka wananchi watumiaji wa barabara hizo kuwa wazalendo kwa kuhakikisha wanazitunza, wanazipenda, na kuzilinda ili ziweze kudumu kwa muda mrefu zaidi na ziweze kutumika kwa vizazi vijavyo. Ujenzi wa Barabara hizo unatarajiwa kukamilika ndani ya Miezi Kumi na Tano (15) kuanzia Oktoba 2,2017.

0 maoni:

Chapisha Maoni