Ijumaa, 6 Oktoba 2017

MADAKTARI BINGWA KUTOKA CHINA WATOA HUDUMA HOSPITALI YA MAFINGA

Posted by Esta Malibiche on Oct 6,2017 IN NEWS
6, 2017 IN NEWS

Madaktari bingwa kutoka China wakiwa katika Picha ya pamoja naWaziri wa mambo ya nje ya nchi,Afrika Mashariki,kikanda na ushirikiano wa kimataifa Balozi Agustine Mahiga na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

Wananchi wa Wilaya ya Mufindi wakiwa katika hafla ya kuwapokea madaktari hao tisa kutoka katika nchi ya Jamhuri ya watu wa China.

 Waziri wa mambo ya nje dr Agustino  Mahiga akizungumza wakati wa hafla ya kuwapokea madaktari kutoka jamhuri ya watu wa China ambao wataka Mafinga kwa takribani siku mbili kutoa huduma kwa wagonjwa mbalimbali na katikati yake ni mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William na Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi
 Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi  akizungumza wakati wa hafla ya kuwapokea madaktari kutoka jamhuri ya watu wa China ambao wataka Mafinga kwa takribani siku mbili kutoa huduma kwa wagonjwa mbalimbali na katikati yake ni mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William na waziri wa mambo ya nje dr Agustino  Mahiga.

 Madaktari 9 kutoka jamhuri ya watu wa china wapo katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kwa ajili ya kusaidia kuwatimu wangonjwa wenye magonjwa sugu na magonjwa yasiyo sugu lakini madaktari hao wamepatikana kwa ushirikiano wa mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi na waziri wa mambo ya nje dr Agustino Mahiga.
Akizungumza na blog hii mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi alisema kuwa lengo na kuja kwa madaktari hao ni kubadirishana uwezo na ujuzi kwa madaktari wazawa ili kuendelea kuboresha sekta ya afya kwa wananchi wa jimbo hilo na wana wanaokuja kupata huduma katika hospitali za Mafinga.
“Hospitali ya Mafinga imekuwa ikihudumia wananchi kutoka halmashauri mbalimbali na mikoa mbalimbali kutokana na jeografia yake ilivyo,hii hospitali ipo katika barabara kuu hivyo wananchi wote wakipata shida ya ugonjwa wowote wanakimbilia hapa hivyo ni lazima tuboreshe sekta ya afya ili kuokoa maisha ya wananchi wetu” alisema Chumi
Chumi ameongeza kuwa madaktari hao watakuwa wakitibu magonjwa yote mfano macho,mifupa,uzazi koo na kadharika hiyo ni faida kubwa kwa wananchi na madaktari wazawa kujifunza au kupata elimu kutoka wa madaktari kutoka nchi ya China.
“Sio kuwa madaktari wetu hawana uwezo ila kujengeana uwezo au kujifunza ni jambo la kawaida hasa katika sekta kama hii ambayo inaumuhimu sana katika maisha ya mwanadamu”alisema Chumi
Naye waziri wa mambo ya nje dr Agustino Mahiga aliwataka viongozi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa madaktari hao kwa kuwa wao ndio wenyeji na wanajua mambo mengiya hapa Tanzania hapa wilaya ya Mufindi kuliko hao madaktari.
“Kiukweli sisi watanzania tunajijua tabia zetu hivyo naomba tufanye yaliyo mema na kuonyesha ushirikiano wa kutosha kutoka kwa hawa madaktari ambao najua tutajifunza kitu kutoka kwao” alisema Mahiga
DR Mahiga alisema kuwa Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano mzuri hivyo yatupasa kuendelea kudumisha ushirikiano huu ambao unafaida kwa nchi zote mbili.
Naye mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliamu aliwakikishia viongozi hao kuwa madaktari hao kutoka jamhuri ya watu wa China watapewa ushikiano mzuri ili wakiondoka wakatoe sifa nzuri

0 maoni:

Chapisha Maoni