Mkurugenzi
wa kapuni ya News Forst Tshepiso Dumasi akitoa risala kwa mgeni
rasmi,katika hafla fupi ya kukabidhi Jengo la vyumba vya madarasa shule
ya Msingi Kimala iliyopo katika kijiji cha Kimala Wilayani Kilolo
Mkoani Iringa.PICHA NA ESTA MALIBICHE.
Na
Esta Malibiche,Majira
Kilolo
WANANCHI wa kijiji cha Kimala ,kilichopo kata ya
Kimala Wilaya Kilolo Mkoani Iringa,wameishukuru kampuni ya News Forest kwa
kuwajengea madarasa mawili kwa ajili ya kusomea watoto wa Shule ya Msingi
Kimala.
Kauli hiyo imetolewa jana na Ezekiel Nyamonga ambae ni
Mwenyekiti wa kamati ya Shule hiyo wakati wa uzinduzi wa vyumba vya
madarasa katika shule ya Msingi Kimala
Wilayani Kilolo, huku akiwataka wanadau wengine wa maendeleo kujitoa hasa
katika setkta ya Elimu ili changamoto
zinazoikabili shule hiyo ziweze kupungua ama kumalizika kabisa.
Nyamonga alisema kuwa hapo awali walikuwa
wanakabiliwa na uhaba wavyumba vya madarasa kutokana na wimbi kubwa la
wanafunzi kuongezeka mara baada ya
serikali kutamka kuwa Elimu bure,wazazi wengi wamekuwa na mwamko na kuwaandikisha
watoto wao.
Bado tunakabiliwa na changamoto ya vyumba vya
madarasa,ninawaomba wadau wa Elimu mjitokeze kutusaidia ili watoto wetu waweze
kusoma wakiwa wamekaa mahali panapostahili,hii itasaidia kuinua kiwango cha
ufauru katika shule yetu’Alisema Nyamonga
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya
Kilolo Asia Abdalah,Katibu Tawala wa Halmashauri
ya Wilaya ya Kilolo Yusuph Magwaya aliwasihi walimu kuahakikisha wanasimamia
swala la ulinzi kwa wananfunzi ili
madarasa waliyokabidhiwa yasiharibiwe.
Magwaya aliwasihi wazazi kuwa karibu na walimu
na kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya
watoto wao shuleni, kuwapunguzia kazi za kufanya pamoja na hatimae kuwapa muda
mwingi wa kujikumbusha masomo wawapo
nyumbani.
'Ninawaomba wawazi hasa akina mama,kuweni karibu
na watoto wenu,acheni tabia ya kuwaachia walimu kila kitu.Ili ndoto zao ziweze
kutimia manatakiwa kukagua masomo yao,kuwapa muda wa kujifunza na kuhakikisha
mnawapa satahiki zao zinazotakiwa kama daftari,karamu nk.’’’Alisema Magwaya
Awali akisoma Risala ya kampuni ya News Forest Mkurugenzi
Tshepiso Dumas alisema kuwa kutokana na kampuni hiyo kutambuau muhimu wa jamii
zinazowazunguka sababu pekee iliyowasukuma kwa kiasi kikubwa sana kuchangia
Kuboresha katika Elimu, hali ya uchumi wa kaya na jamii kwa ujumla huku kushirikiana
na wadau mbalimbaliwa maendeleo.
Dumas alisema kwa kiasi kikubwa shughuli zetu za
kijamii zinafanikiwa kutokana na ushirikiano mkubwa kukota katka Serikali ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia viongozi wake wa nchi, mikoa, wilaya,
Tarafa, kata na vijiji pamoja na jamii kwa ujumla. Na kuongeza kuwa katika Mradi
huo wa ujenzi wa vyumba vya madarasa wamefanikiwa kwa asilimia kubwa, hii ni
kutokana na ushirikiano mkubwa uliokuwepo kati ya viongozi wa serikali, kijiji
na jamii kwa ujumla.
‘’ Ndugu mgeni rasmi, Kampuni ya New Forests
ilianza rasmi kufanya kazi hapa nchini Tanzania mwaka 2010, inajishughulisha na
misitu na inafanya kazi katika nchi za jangwa la Saraha, ambapo
inajishughulisha na uuzaji wa nguzo za umeme zilizotibiwa, pia inapanda miti ya biashara ikiwemo Miringoti
(Eucalyptus) na Misindano (Pine).Pia Kampuni ya New Forest imepata umaarufu mkubwa
katika kukuza sekta ya ujenzi, Miundo
mbinu na sekta ya umeme Mashariki na
Kusini mwa Africa kwa bidhaa za mbao na nguzo za umeme zenye kiwango cha
hali ya juualisema Dumas na kuongeza kuwa
Mradi huu wa ujenzi
wa vyumba vya madarasa umegharimu pesa za kiasi cha milion 48,707,340.Kampuni
imechangia kiasi cha milioni 44,279,400 katika ujenzi wa jengo ambalo ni sawa
na asilimia 90.{90%),jamii imechangia kiasi cha milioni 4,427,940 malighafi za
ujenzi ambayo ni sawa na asilimia 10 (10%)na wilaya imechangia kupendekeza mwalimu
aliyehusika katika utekelezaji wa Mradi’’Alisema Dumas
Ninapenda kuwapongeza
wananchi wa kijiji cha kimala kwa ushirikianowao mkubwa waliouonyesha wakati wa
utekelezaji wa Mradi, kwa hakika hakukuwa na changamoto yoyote tangu tulipoanza
ujenzi hadi tumemaliza na hatimae
kuukabidhi kwa wananchi hii leo.
Aliongeza kuwa Mradi huo ulianza kutekelezwa mwezi
wa nane mwaka 2016 na ulikamilika mwezi wa kumi na mbilimwaka 2016.,wakiwa na
lengo la kukidhi uhaba na uchakavu wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo ya
msingi kama jamii ilivyopendekeza kipindi cha mipango shirikishi ya jamii.
Kampuni
inapendakuwasihi walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kimala kuyatunza madarasa
haya ili yawe msadda
kwaos asa na kwa vizazivijavyo.Pia tunapenda kuishukuru Halmashuri ya Wilaya ya
Kilolo kwa ushirikiano walioutoa katika kutekeleza shughuli zetu ikiwa nipamoja
na mradi huu.
|
Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo,Yusuph Magwaya akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo,Asia Abdalah.PICHA NA ESTA MALIBICHE.
|
Wanafunzi
wa shule ya Msingi Kimala wakishiriki hafla ya kukabidhiwa jengo la
vyumba vya madarasa yaliyojengwa na wadau wa maendeleo ambao ni Kampuni
ya New Forests
|
|
|
0 maoni:
Chapisha Maoni