Posted by Esta Malibiche on Oct 12,2017 IN NEWS
Wananchi wa kijiji cha Kising'a Wilayani Kilolo Mkoani Iringa wakiwa katika hafla fupi ya kukabidhiwa nyumba ya wauguzi wa Zahanati ya Kising'a iliyojengwa na Kampuni ya New Forests.PICHA NA ESTA MALIBICHE.
Mkurugenzi wa kapuni ya New Forests, Tshepiso Dumasi akitoa risala kwa mgeni rasmi,katika hafla fupi ya kukabidhi nyumba ya wahudumu wa Afya wa Zahanati ya Kising'a iliyopo katika kijiji cha Kising'A Wilayani Kilolo Mkoani Iringa.PICHA NA ESTA MALIBICHE.
Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo,Yusuph Magwaya akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo,Asia Abdalah.
Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo,Yusuph Magwaya akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo,Asia Abdalah. |
Na Esta Malibiche
Kilolo
Wananchi wa kijiji
cha Kising’a Wilayani Kilolo Mkoani Iringa wametakiwa kutunza nyumba ya wauguzi
wa
zahanati ya kijiji hicho iliyokabidhiwa na Kampuni ya New Forest jana
ili iweze kuwasaidia watumishi hao
waliokuwa wanakabiliwa na chanagamoto ya kukaa mbali na kituo cha kazi hivyo
kushindwa kuwahudumia wananchi kwa wakati.
Kauli hiyo imetolea
jana na Meneja rasilimali watu Sara Tesha wakati akisoma risala ya kampuni hiyo
kwa Mgeni Rasmi wakati wakikabidhi Nyumba wa wauguzi wa Zahanati ya Kising’a iliyopo
katika kijiji cha Kising’a Wilayani Kilolo Mkoano hapa.
Katika Risala yake alisema kuwa kampuni hiyo kwa
kutambua umuhimu wa jamii zinazowazunguka
ndiyo maana imewekeza kwa kiasi kikubwa sana katika kuchangia Kuboresha Afya, hali
ya uchumi wa kaya na jamii kwa ujumla.
Tesha alisema kuwa Mradi huo umegharimu pesa za
kitanzania milion 51,168,000. hata hivyo Kampuni imechangia Tsh. i 46,051,200 Mill.katika
ujenzi wa jengo hilo,ambayo ni sawa na asilimiatisini (90%), jamii imechangia
Tsh. Mill 5,116,800 malighafi za ujenzi ambayo ni sawa na asilimia 10 (10%)na
wilaya ya Kilolo imechangia kupendekeza muudumu wa afya aliyehusika katika
utekelezaji wa Mradi huo.
‘’Lengo la Mradi huu ni kukidhiu haba wa nyumba
za wauguzi katika Zahanati hii ya kising’a kama jamii ilivyopendekeza kipindi cha
mipango shirikishi ya jamii ambapo kwa kiasi kikubwa shughuli zetu za kijamii zinafanikiwa
kutokana na ushirikiano mkubwa kukota katka Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia viongozi wake wa nchi, mikoa, wilaya, Tarafa, kata na vijiji
na jamii kwa ujumla.
Alisma Katika Mradi huu wa ujenzi wa nyumba ya
wauguzitumefanikiwa kwa asilimiazote hii ni kutokana na
ushirikianomkubwauliokuwepokati ya viongozi wa serikali, kijiji na jamii kwa
ujumla na kuongeza kuwa
Kilapenyemafanikiohapakosi
changamoto, changamoto kubwatuliyoipata katika utekelezaji wa Mradi huu ni utayarimdogo
wa jamii katika kuchangia asilimia 10 (10%). Tulifanikiwa kutatua changamoto
hii kwa kuielimisha jamii umuhimu wa Mradi na umiliki wa mradi. Baada ya Elimu
jamii ilielewa na kuchangia hata kukamilika kwamradi huu
Kwa upande wake
katibu Tawala wa Wilaya ya Kilolo,Yusuph Magwaya aliishukuru Kampuni ya New
Forests kwa kujitolea ujenzi wa nyumba hiyo na kusema kuwa imetatua changamoto ya hapo awali ambapo wauguzi waliokuwa wanakaa mbali na kituo cha
kazi hivyo kushindwa kuwahudumia wananchi
ipasavyo.
‘Mara nyingi
tumekuwa tukilalamika kuwa wahudumu wa
Zahanati wanakaa mbali na kituo ,Leoa hii tumepata nyumba kutoka Kampuni ya
New Forests na tuaanza kuhudumia vizuri,ninawaomba tuwe walinzi kuhakikisha
wale wataokaa hapa wanaitunza hii nyumba ili na wengine wakija waikute’Alisema
Magwaya
Pia alisisitiza
swala la vyoo bora kwa kuwahamasisha wananchi kuhakikisha wanakuwa na vyoo
hivyo ili kujikinga na magonjwa ya amlipuko,kama kipindupindu na magonjwa
mengine.
Aidha aliwataka wanachi kuyatunza mazingira kwa
kutochoma moto ovyo katika misitu iliyopandwa na kuhidfadhiwa .
0 maoni:
Chapisha Maoni