Jumamosi, 7 Oktoba 2017

DIWANI CHADEMA AJIUNGA NA CCM IRINGA

Posted by Esta Malibiche on Oct 7,2017 IN SIASA

Aliyekuwa Diwani wa kata ya Kitwiru kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,Baraka Kimata na wenzake,wamejitoa Mapema leo hii  katika chama hicho,n na kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Iringa Mjini.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumkabidhi Mwenyekiti wa CCM Iringa Mjini kadi ya Chadema na kukabidhiwa Kadi ya chama cha Mapinduzi CCM katika ofisi za CCM Iringa Mjini alisema kuwa,amechoshwa na Demokrasia mbovu ya Chadema isiyo na uzalendo wa kweli  katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Ninawaomba watanzania wasiyumbishwe na aiasa za uongo kutoka Chadema ,chama kisicho na katiba wala dira pia hakina mwelekeo zaidi ya maslai yao.

"Ninawaomba mjiunge na CCM inayofanya kazi kubwa ya kuqatumikia wqnanchi kwq kuhakikisha rasilimali zilizopo Nchini zinaqanufaisha wananchi.Alisema Kimata na kuongeza kuwa

Kwakutambua mchango mkubwa unaofanywa na Mh.Rais Mgufuli,nimeona nijiunge CCM kwa lengo la kuunga mkono kwa vitendo juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt.John Joseph Magufuli.

"Sisi sote ni Mashuhuda tunaona juhudi za dhati zinazofanywa na Mh.Rais wetu kipenzi cha watanzania.Ninawaomba tumuunge mkono kwa nguvu zote kwa umoja wetu" Alisema Kimata

Alisema atashirikiana na viongozi wa CCM kuhakikisha kata ya Kitwiru ambayo iko wazi kwa sasa anahakikisha inarejea ndani ya CCM huku akiahidi chama cha Mapinduzi kinashinda kwa kishindo.
Aliyekuwa Diwani wa kata ya Kitwiru kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,Baraka Kimata na wenzake,wamejitoa Mapema leo hii  katika chama hicho,n na kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Iringa Mjini.
 Mweyekiti wa chama cha mapinduzi  CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya akizungumza  wakati wa kuwapokea wanachama wapya kutoka chama cha demokrasia na maendeleo manispaa ya Iringa akiwa sambamba na viongozi wa chama katika ofisi za CCM wilaya  .


Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Iringa Mjini akizungumza mara baada ya kuwapokea wanachama wapya waliojiunga na chama hicho.



Mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM Iringa Mjini,Salvatory Ngerera akizungumza mara baada ya kuapishwa wanchama wapya waliojiunga na chama cha Mapinduzi leo hii.
 Katibu wa itikadi na uenezi  wa chama cha mapinduzi  CCM Iringa mjini,Edward Bashiri wa kwanza kulia akiwa na wanachama wapya,katikati ni Baraka Kimata aliyekuwa katibu mwenezi wa chadema na Diwani wa kata ya Kitwiru ambaye amejiunga rasmi na CCM na Raymond kimata aliyekuwa kiongozi wa redbrigad manispaa ya Iringa na katibu mwenezi wa kata ya kitwiru wote wawili wamejiunga leo na chama cha mapinduzi.

Wanachama wapya wakila kiapo















0 maoni:

Chapisha Maoni