Posted by Esta Malibiche On Oct 25,2017 IN NEWS
Katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa manispaa mwl. Fortunata Njalale akizungumza neno wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho manispaa ya Iringa uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.
Mwenyekiti wa chama
hicho manispaa ya Iringa MWL. Zawadi Mgongolwa akizungumza neno wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho manispaa ya Iringa uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa akiwa sambamba na katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka.
Baadhi ya walimu waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa
Chama cha walimu wa Tanzania
(CWT) halmashauri ya manispaa ya Iringa kimemuomba mkurugenzi kuwakopesha
viwanja walimu ili kujikwamuamua na mazingira magumu wanayokumbana katika
nyumba wanazoishi.
Akisoma risala ya katika mkutano
mkuu wa chama hicho manispaa ya Iringa katibu wa chama cha walimu wilaya ya
Iringa mwl. Fortunata Njalale alisema kuwa walimu wamekuwa wakiishi katika
nyumba chakavu au mbali na mazingira ya shule kitu kinachosababisha kushuka kwa
uwezo wa walimu kufundisha.
“Unamkuta mwalimu anakaa
kihesa kilolo lakini anafundisha shule ya Tagamenda sasa ukiangalia umbali ni
mrefu sana hiyo yote kutokana na kutokuwa na makazi katika eneo husika hivyo tunaomba
kukopeshwa viwanjwa ili na sisi walimu tumiliki nyumba zetu” alisema Njalale
Njalale alisema kuwa walimu
hawana pesa za kununua moja kwa moja viwanja hivyo kwa njia ya kuwakopesha
inawezekana kutokana kuwa ni waajiliwa wa serikali na mishahara yao inajulikana
na ni rahisi kuresha mkopo huo.
“Sisi walimu ukitaka kujua
mimi nalipwa shilingi ngapi ni rahisi tu kwa kuwa mishahara ya serikali mara
nyingi inajulikana hasa pale mtumishi unapoenda kukopa mahali ndio maana
tunaiomba serikali itusaidie kukopa viwanja kuwa kuwa tunauwezo wa kulipa kwa
awamu tatu” alisema Njalale
Aidha Njalale alimwambia
mgeni rasmi kuwa ombi la walimu wa halmashauri ya manispaa ya Iringa ni la muda
mrefu hivyo wanamuomba alishughulikie ili walimu waweze kupata viwanja hivyo
kwa nao wajenge nyumba zao.
“Njalale alisema kuwa walimu
wanalipwa mishahara midogo lakini wanapanga nyumba kwa gharama kubwa kutokana
na mazingira ya mjini yalivyo na bila kumsaidia walimu kutasababisha
kutengeneza taifa lisilokuwa na wasomi wenye tija ya kuleta maendeleo” alisema Njalale
Akijibu risala hiyo katibu
tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka aliwataka uongozi wa walimu
kuandika barua ya kuomba viwanja ili waweze kulishughulikia swala hilo likiwa
kwenye maandishi.
“Andikeni barua yenye idadi
na majina ya walimu wanaotaka viwanja ili kuondoa kasumba ya kusema wanaotaka
ni kikukindi cha walimu wachache tu na bila kufanya hivyo swala lenu la kuomba
viwanja litakuwa gumu kulitafutia ufumbuzi” alisema Chintinka
Chintinka aliwaomba walimu
wawewavumilivu katika kipindi wacholishughulikia swala hilo kwa kuwa sio jambo
la kukurupuka linahitaji utulivu wa kutosha ili kufanikishwa swala walimu kupata
viwanja.
0 maoni:
Chapisha Maoni