Jumatano, 25 Oktoba 2017

DC MOFUGA:VIJANA WANAOJIUNGA NA JKT LAZIMA WAPITIE MAFUNZO YA MGAMBO

Posted by Esta Malibiche on Oct 25,2017 IN NEWS

Mkuu wa wilaya ya Mbulu mkoani Arusha Chelestino Mofuga akixungumza na vijana 171 wakati wa kufungua mafunzo ya mgambo mapema leo hii wilayani uumo.

Mkuu wa wilaya ya mbulu Mkoani Arusha chelestino  s Mofuga leo 25/10/2017 amezindua mafunzo ya jeshi la akiba ,ambapo jumla ya wanafunzi 171 wanaendelea na mafunzo. 

Akiongea na wananchi na wanafunzi hao mkuu wa wilaya ameagiza askari wanaolinda maeneo mbalimbali na hasa biashara na ofisi mbalimbali ni lazima wawe wamepita mafunzo hayo, amesisitiza kwamba ni marufuku raia kuajiliwa kama walinzi ili vijana hao waweze kupata ajira. Pia ameagiza vijana wanaojiunga na Jkt ni lazima wapite   mafunzo ya mgambo .

Mofuga amewapongeza wananchi kuitikia wito wa kwa kuwaruhusu vijana kuingia mafunzo hayo.

 Mkuu wa wilaya ametumia muda huo kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha kupata vitambulisho vya Taifa
Mkuu wa wilaya ya Mbulu mkoani Arusha akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Mgambo wilayani humo.

Mkuu wa wilaya ya Mbulu mkoani Arusha Chelestino Mofuga akixungumza na vijana 171 wakati wa kufungua mafunzo ya mgambo mapema leo hii wilayani humo.



0 maoni:

Chapisha Maoni