Ijumaa, 9 Februari 2018

WAZIRI WILLIAM LUKUVI AKABIDHI KOMPYUTA 25 KWENYE SHULE ZA SEKONDARI ZA JIMBO LAKE

Posted by Esta Malibiche on FEBRUARI 9,2018   

 Mbunge wa jimbo la Isman na waziri wa ardhi nyumba na makazi Wiliamu Lukuvi ametabidhi jumla ya kompyuta ishirini na tano (25) kwenye sekondari za jimbo hilo kwa lengo la kuboresha elimu kwa wanafunzi ili kuendana na teknolojia ya sasa.
 Mbunge wa jimbo la Isman na waziri wa ardhi nyumba na makazi Wiliamu Lukuvi ametabidhi jumla ya kompyuta ishirini na tano (25) kwenye sekondari za jimbo sita za jimbo lake
 Mbunge wa jimbo la Isman na waziri wa ardhi nyumba na makazi Wiliamu Lukuvi ametabidhi jumla ya kompyuta ishirini na tano (25) na hapa akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa sekondari ya Ilambilole
 Mbunge wa jimbo la Isman na waziri wa ardhi nyumba na makazi Wiliamu Lukuvi ametabidhi jumla ya kompyuta ishirini na tano (25) kwenye sekondari za jimbo hilo kwa lengo la kuboresha elimu kwa wanafunzi ili kuendana na teknolojia ya sasa.
Mbunge wa jimbo la Isman na waziri wa ardhi nyumba na makazi Wiliamu Lukuvi ametabidhi jumla ya kompyuta ishirini na tano (25) akiwa na mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Isman


Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mbunge wa jimbo la Isman na waziri wa ardhi nyumba na makazi Wiliamu Lukuvi ametabidhi jumla ya kompyuta ishirini na tano (25) kwenye sekondari za jimbo hilo kwa lengo la kuboresha elimu kwa wanafunzi ili kuendana na teknolojia ya sasa.
 
Akizungumza katika shule ya sekondari Ilambilole Lukuvi alisema kuwa ameamua kutafuta njia ya kuendelea kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa kompyuta ambazo zitawasaidia walimu na wanafunzi kujua kuwa ulimwengu unaendaje.

“Saizi tunasema kuwa dunia ipo kiganjani kwako hivyo sekondari zangu zisipokuwa na kompyuta itakuwa nyuma kiteknolojia hivyo anafanya kila liwezekalo kuhakikisha shule zote za jimbo la Ismani zinaendana na sayansi na teknolojia” alisema Lukuvi

Lukuvi aliwata walimu kufanya kazi kwa kujituma kuhakikisha wanafunzi wanafaulu kwa wingi na kuifanya elimu katika jimbo hilo kuwa yenye ubora unaostahili na kuwa kivutio kwa wananfunzi wengine kukimbia kusoma katika shule hizo.

“Kweli mnafanya vizuri sana lakini naombeni muongeze bidii kuhakikisha shule hizi za sekondari za jimbo la Ismani zinakuwa za mfano kwa kutoa elimu bora na mkifanya hivyo mbunge wenu mnanijua nitakikisha nawatafutia zawadi nzuri kwa maendeleo ya kwenu na wanafunzi mnaowafundisha” alisema Lukuvi

Aidha Lukuvi alimpongeza rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kazi kubwa anaifanya ya kuhakikisha kuwa wananchi wanaofanya kazi wanapata kile wanachostahili na kuondoa dhana ya kuishi kimazoea kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Saizi usipofanya kazi huwezi pata chochote kile hivyo nilazima kila mwananchi awajibike kwenye maeneo yake kwa kufanya kazi ili apate kipata la sivyo wataishia kulalamika kila siku nawaambieni ukweli” alisema Lukuvi

Lukuvi aliongeza kuwa ataendelea kutafuta pesa kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa majengo ya shule hizo kadri atakavyokuwa amepata fursa hiyo ila akawaomba wananchi na viongozi kutunza miundombinu ambayo inakuwa imejengwa na wafadhili ili itumike kwa miaka mingi.

Nao baadhi ya wakuu wa shule ya sekondari ya Ilambilole na Ismani walimshukuru mbunge huyo kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha anaboresha sekta ya elimu.

“Angekuwa mbunge mwingine asingehangaika kuhakikisha anaboresha sekta hii lakini huyu mbunge wetu Lukuvi amekuwa msaada sana kwa walimu kwa kutoa misaada mbalimbali hivyo tunamuombea kwa mungu amjalie aendele kuwa na  afya njema” walisema walimu
SHARE: 

0 maoni:

Chapisha Maoni