Jumatatu, 26 Februari 2018

KILIMO, VIWANDA VYAINUA PATO LA MKOA WA IRINGA



Posted by Esta Malibiche on Februari 26,2018 in NEWS

Image result for MKUU WA MKOA WA IRINGA AMINA MASENZA
Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Amina Masenza akizungumza na Wandishi wa Habari[hawapo pichani]kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu.

MKUU wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amesema kuwa Sekta ya kilimo na viwanda inaendelea kwa kasi Mkoani hapa,huku ikichangia kuongezeka kwa pato la Mkoa kutoka Sh trilioni 2.3 mwaka 2010 hadi  kufikia Sh trilioni 5.10 mwaka 2016.

Akizungumza na wandishi wa Habariofisini kwake,  alisema; “pato la Mkoa huchangiwa kwa kiasi kikubwa na mashamba makubwa ya chai, misitu na tumbaku pamoja na viwanda vya  vyake.”

Alisema ongezeko hilo limenyanyua pia pato la mkazi kutoka Sh Milioni 1.3 mwaka 2010 hadi Sh Milioni 2.9 mwaka 2016.

Alisema sekta ya kilimo mkoani Iringa ni muhimili mkuu wa uchumi na inachangia katika usalama wa chakula na utoaji wa ajira.

“Sekta hii inachangia takribani asilimia 85 ya pato la mkoa wa mujibu wa wasifu wa kiuchumi na kijamii wa mkoa wa mwaka 2013,” alisema.

Alisema lengo la mkoa ni kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na chakula cha kutosha, kipato cha kaya kinaongezeka na kilimo kwa kusaidiana na viwanda vinaendelea kuwa muhimili mkuu wa uchumi.

Alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana, mkoa ulikuwa na jumla ya viwanda 695 kati yake vikubwa vikiwa 24, vya kati 35, vidogo 149 na vidogo zaidi 1,995.

“Sekta hii ya viwanda inaajiri watu takribani 15,000 sawa na asilimia 1.6 ya wakazi wa mkoa wa Iringa kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012,” alisema.

Akizungumzia kampeni ya uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda mkoani humo kama sehemu ya utekelezaji wa azma ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda, alisema kila halmashauri inatakiwa kujenga viwanda visivyopungua 35 mwaka huu.

Katika kufanikisha azma hiyo alisema mkoa umeunda timu ya uratibu yenye wajumbe 18 wakiwemo wataalamu kutoka vyuo vikuu vya mkoani Iringa, sekretarieti ya mkoa pamoja na sekta binafsi.



0 maoni:

Chapisha Maoni