Alhamisi, 8 Februari 2018

JAFO ASHUSHA NEEMA YA LAMI KM 3 BABARA YA CHANG’OMBE MANISPAA YA DODOMA MJINI,AMFAGILIA MBUNGE MAVUNDE KWA KAZI YA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI

Posted by Esta Malibiche on Februari 8,2018 IN NEWS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa Soko la wafanyabiashara wadogo wadogo wa Chang'ombe Manispaa ya Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.Binilith Mahenge akizungumza katika uzinduzi wa Soko la wafanyabiashara wadogo wadogo wa Chang'ombe Manispaa ya Dodoma.
 Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa Soko la wafanyabiashara wadogo wadogo wa Chang'ombe Manispaa ya Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali katika uzinduzi wa Soko la wafanyabiashara wadogo wadogo wa Chang'ombe Manispaa ya Dodoma


jiwe la msingi la soko la Chang'ombe

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe.Seleman Jafo akitembelea soko la Chang'ombe mara baada ya kuzindua.

 Wafanyabishara wa Soko la Chang'ombe Manispaa ya Dodoma
Baadhi ya bidhaa zilizopo soko la Chang'ombe



WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mh Suleiman Jaffo leo amezindua soko la Wafanyabiashara ndogo ndogo Chang’ombe Dodoma kwa kuitaka Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuweka miundombino mizuri katika maeneo ya masoko na kuboresha maeneo hayo ili yaendane na hadhi ya Dodoma,ambapo ametumia fursa hiyo kuwaahidi wakazi wa Chang’ombe juu ya ujenzi wa km 3 wa barabara za lami zitakazounganisha kata ya Chang’ombe na kata nyinginezo.


Mh Jaffo ameyasema hayo leo kata ya Chang’ombe alipokuwa akizindua soko lenye thamani ya Ts 70,000,000 lililojengwa kwa ushirikiano wa Wafanyabiashara wa Soko,Mbunge wa Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde na Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.

Kwa wakati mmoja,Waziri Jaffo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Benilith Satano Mahenge wamempongeza Mbunge Anthony Mavunde kwa kazi kubwa anayofanya ya kuwaletea wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini maendeleo na kuwataka wananchi wa Dodoma kumuunga mkono Mbunge wao.

0 maoni:

Chapisha Maoni