Jumatatu, 5 Februari 2018

MWIGULU NCHEMBA:KAMATENI WAHARIFU WOTE WANAOINGIZA MIZIGO NCHINI KIMAGENDO

Posted by Esta Malibiche ON FEBRUARI 52018  IN NEWS

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa kwani taasisi hiyo ndiyo inayoshughulika na haki za watu moja kwa moja na wasipofanya kwa uadilifu ina madhara  makubwa kwa jamii na kutoka kwa wahalifu.

Akizungumza  katika uzinduzi wa ujenzi wa Kituo cha polisi Wilaya ya Pangani leo, Dk Mwigulu alisema kuwa wilaya ya pangani ni lango ambalo wahalifu hasa wahamiaji haramu upitia kwenda kusini mwa Tanzania. 

‘’kamateni wahalifu wote wote wanaingia kimagendo au wanaoingiza mizigo kimagendo hakuna mjadala kamateni na wafikisheni katika vyombo vya sheria ,’’alisema Dk Mwigulu.

Kwa mujibu wa Dk Mwigulu, Mikoa ya kaskazini mwa Tanzania inaongoza kwa kuingiza wahamiaji haramu na bidhaa kwa magendo kwasababu ipo mipakani.

‘’Ujenzi huu wa kituo cha polisi utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama zaidi hivyo mimi nitachangia nondo 150 baada ya mifuko 450 ya cement kupatikana basi ujenzi uanze haraka iwezekanavyo na kituo kiwe cha hali ya juu kikubwa.’’ alisisitiza.

Kwa upande wake, Mkuu wa polosi Wilaya hiyo, Mrakibu Mwandamizi wa polisi Christina musyani alisema kuwa wilaya hiyo inavituo vitatu pekee vya polisi ambavyo havitoshi na mazingira yake hayaridhishi.

Alisema wameamua kuanza ujenzi wa kituo hicho ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wakazi wa eneo hilo ambao kwa sasa hulazimika kusafiri umbali mrefu kutafuta vituo vya polisi.

‘’Kwa kushirikiana na wananchi, mbunge na halmashauri tumeamua kuanza ujenzi wa kituo cha kisasa ,’’ alisema Christina.

Naye mbunge wa jimbo la Pangani Juma Uwesu amesema yeye wakati anagombea ubunge alihaidi kuwatetea  vyombo vya ulinzi  na usalama kupata makazi mazuri na maslai mazuri hivyo yeye atatoa mifuko 200 huku mkuu wa mkoa na halmshauri ya pangani ikitoa mifuko 250 kuanza ujenzi huo.

Waziri Dk Mwigulu yupo ziara ya kikazi wilaya ya pangani kwa siku mbili kukagua utendaji kazi wa idara zilizopo chini ya wizara yake na kukagua maeneo ambayo wahamiaji haramu na bidhaa za magendo zinapita.​



















0 maoni:

Chapisha Maoni