Jumamosi, 10 Februari 2018

SERIKALI YAIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOLO MKOANI IRINGA KWA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

Posted by Esta Mlaibiche on FEBRUARI 10,2018 IN KITAIFA
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika kwakati wa kikao cha kupokea taarifa ya Wilaya ya Kilolo ikiwa siku ya pili ya ziara yake mkoani Iringa, wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Venance Mwamoto (kulia) naMnecwa Mkoa wa Iringa,ambae pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Bw. Salim Abri Asas. 
 Esta Malibiche
Kilolo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu,amesema Serikali inaendelea  kujipanga kuhakikisha inatekeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara wilayani Kilolo Mkoani hasa barabara inayounganisha Kilolo na Mkoani Iringa kupitia Ipogolo yenye urefu wa km 25.

Hayo ameyasema mapema leo hii wakati akizungumza na watumishi wa Serikali wa Halamashauri ya Wilaya ya Kilolo Mkoani hapa,alisema kuwa barabara hiyo ipo kwenye Ilani  ya Chama cha Mapinduzi,hivyo Serikali inayoongozwa na CCM haina budi kutekeleza.

Akizungumzia sekta ya Afya, Maji na Elimu alisema kuwa Serikali inaendelea kuyabeba kwa nguvu zote sababu ili Tanzania  iwe nchi ya Viwanda lazima Serikali ihakikishe Maji safi na salama yanapatikana,wananchi wanakuwa na  Afya bora,pia waweze kupata Elimu stahiki,ndiyo maana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejielekeza katika inatekeleza kwa vitendo huduma hizo.

Makamu wa Rais aliipongeza Halmashauri ya Kilolo kwa kupiga hatua katika amaendeleo ikiwa nipamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inatotolewa na Serikali.

Aidha Makamu wa Rais akiwa Wilayani Kilolo,amezindua ujenzi na ukarabati wa jengo la utawala katika Shule ya Sekondari Kilolo uliogharimu kiasi cha Tsh. 151 Mill.,ambapo wananchi wametoa kiasi cha Tsh.15 Mill. na Tsh.136 Mill zimetolewa na Serikali kuu.Pia alizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kilolo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Mji mdogo wa Ilula. 

Awali Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Abdalah akisoma taarifa ya utekelezaji wa Shughuli za Maendeleo wilayani humo alisema kuwa,Wilaya aya Kilolo katika kutekeleza majukumu yake imeweza  kufanikiwa kukusanya mapato yake ya ndani kiasi cha Tsh.2,319,546,666.07 kati aya makisio Tsh.2,807,761,275.oo sawa na asilimia 82.61 katika mwaka wa fedha 2016/2017.

‘’Mheshimiwa makamu wa Rais, mafanikio haya yamepatikana kutokana na  kutumia mfumo wa kielekroniki katika ukusanyaji wa mapato ya ndani.Pia kiwango cha   uptikanaji wa maji vijijini kimeongezeka  kutoka asilimia 71,kwa mwaka2o16/2016 kutoka asilimia 57.9 kwa mwaka 2013/2014’’Alisema Asia

Asia alisema  kuwa wamefanikiwa kuwezesha kuwepo mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji 35 na upimaji na utoaji wa hati miliki za kimila 850 kwa wananchi.

Aliongeza kuwa wilaya ya Kilolo imepokea kiasi cha Tsh.400,00o,000,00 kwa ajili ya ukarabati wa  kituo cha Afya kidabaha na jamii husika itashirikishwa kuhakikisha wanatekeleza na hatimae mradi huo kukamilika.

Tumeweza kuboresha miundombinu ya ya barabara kwa kutengeneza jumla ya km.137,amabpo matengenezo ya kawaida ni km 73,matengenezo ya muda maalum km 28,matengenezo ya sehemu korofi km38 na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ni km 4.4’’Alisema Asia na kuongeza kuwa

Ili kuhakikisha wananchi wanajikwamua kiuchumi Halmashauri inaendelea na mikakati  ya kufufua mashamba na kujenga kiwanda cha Chai katika eneo la dabaga,pamoja na kuwahamasisha wananchi kuhusu uanzishwaji wa viwanda vidogovidogo,vya kati na vikubwa vitakavyopelekea kuongeza ajira ,kukua kwa kipato cha wananchi na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu anaendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Iringa,ambapo kesho atakuwa Wilayani Mufindi kukagua shughuli za Maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Juma Abdallah akiasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za amaendeleo wilayani humo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua  jengo la Utawala la shule ya sekondari ya Kilolo Mkoani Iringa.​
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa B. Amina Masenza wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la Utawala la shule ya sekondari ya Kilolo mkoani Iringa. 
 






















0 maoni:

Chapisha Maoni