Posted by Esta Malibiche on februari 5,2018 IN NEWS
Meneja wa NSSF Mkoa wa Iringa Josephat Komba akizunguumza na wanajeshi wastaafu katika kikao kilichofanyika mkoani Iringa na kuhudhuliwa na Mwenyekiti wa Chama cha wanajeshi wastaafu MUWAWATA.
Na Esta Malibiche
Iringa
WANAJESHI wastaafu mkoani Iringa wametakiwa kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii wa (NSSF) kwa lengo la kupata matibabu
badala ya kutumia fedha nyingi pindi wanapostaafu.
Kilio hicho kimekuja mara baada ya kuona wanateseka
kupata matibabu kutokana na hali duni ya kipato wanachokipata pindi
wanapostaafu.
Akizungumza mapema leo hii na baadhi ya wanajeshi hao kwenye ukumbi wa
hol fare uliopo mkoani Iringa Meneja wa NSSF mkoa wa IringamJosephat Komba alisema
kuwa lengo la NSSF inatoa huduma ya
matoibabu kwa wanachama kwa bei nafuu,ambapo kila Mwanachama anatakiwa
kuchangia kiasi cha Tsh.20
elfu,ukilinganisha na kutibiwa kwa kawaida.
Akizungumzia hali halisi ya wanajeshi wastaafu ambao
wanaendelea kusubiri mafao yao alisema kuwa mpaka sasa waliokamilisha usajili
ni wanachama 67 pia wanachama 22 fomu zao zipo kwenye mchakato wa kusajiliwa.
‘’Malengo yetu kama NSSF kwa Mkoa wa Iringa ni kufikia
wanachama 500.Kwa sasa mwamko wa wanajeshi wastaafu kujiunga ni mdogo tunaendelea
kutoa Elimu kpitia muunganiko wao ili waweze kujiunga
Komba alisema kuwa NSSF
inatoa mafao mbalimbali kwa
wastaafu yakiwemo Mafao ya
matibabu,Fao la msaada wa mazishi kwa kugharamia mazishi yote ndani ya Mkoa husika.Pia katika
msaada wa mazishi mtu anaehudumiwa ni
yule aliyejiunga tu na si vinginevyo,pamoja na fao la urithi’’Alisema Komba
Asseid Mayugi
ni Mwenyekiti wa Chama cha wanajeshi wastaafu Muwawata,akizungumza alisema kuwa
wanajeshi hao wamekuwa ajili ya matibabu matibabu badala ya kutumia fedha nyingi katika matiabau ukilinganisha na hali duni ya
kipato walichonacho.
Mayugi alisema kuwa hali ya wanajeshi wastafu kwa sasa ni duni hivyo wanashindwa
kupata matibabu kutokana na gharama kubwa ,hivyo aliwataka kujiunga na mfuko wa
Nssf ili waweze kupata matibabu kwa bei nafuu.
Mayugi alisema kuwa
wanajeshi hao wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu tasngu kustaafu
kwao kutokana na hali ya kiuchumi ambapo kwa hivi sasa hutumia pesa nyingi
katika matibabu.
Kwa upande wake,katibu wa Muwawata Auguto Sabagi
alisema kuwa wastafu wajeshi wanatakiwa
kusaidiwa kutokana na Mchango wao walioufanya kwa Taifa.
‘’Ninawaomba wanajeshi wajiunge na chama hiki ili
waweze kunufaika na fursa zinazopatikana’’Alisema Sabagi
Meneja wa NSSF Mkoa wa Iringa Josephat Komba akizunguumza na wanajeshi wastaafu katika kikao kilichofanyika mkoani Iringa na kuhudhuliwa na Mwenyekiti wa Chama cha wanajeshi wastaafu MUWAWATA
Mwenyekiti wa Chama cha wanajeshi wastaafu MUWAWATA,Asseid Rajabu Mayugi akizunguumza na wanajeshi wastaafu katika kikao kilichofanyika mkoani Iringa na kuhudhuliwa na Mwenyekiti wa Chama cha wanajeshi wastaafu MUWAWATA
Wanajeshi wastaafu wakiwa katika kikao
0 maoni:
Chapisha Maoni