Jumatano, 7 Februari 2018

WAZIRI JAFO AWATAKA WADAU WA ELIMU KUUNGA MKONO SERA YA ELIMU BILA MALIPO

Posted by Esta Malibiche ON FEBRUARI 7,2018 IN NEWS

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa mpango maalum wa kusaidia wanafunzi wenye uhitaji maalum ambao ameupa jina la “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akikabidhi madaftari kwa wanafunzi  na uzinduzi wa mpango wa “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akikabidhi madaftari kwa wanafunzi  na uzinduzi wa mpango wa “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akikabidhi madaftari kwa wanafunzi  na uzinduzi wa mpango wa “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.
Wanafunzi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo 
      ..........................................................

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo amewataka Wadau wote wa Elimu pamoja na jamii kwa ujumla kushirikiana na serikali  kutekeleza sera ya elimu Bila Malipo. 

Jafo ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi vifaa vya shule katika shule ya msingi Uguzi, iliyopo wilayani Chamwino, mkoani Dodoma. 

Vifaa hivyo vilitolewa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo Dkt. Ombeni Msuya na Abdala Jacob kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma.

Amewataka wadau hao wasikate tamaa kuunga mkono Serikali kuhusu Elimu.

 “Japo changamoto ni nyingi lakini wanafunzi wenye uhitaji maalum wanahitaji msaada wao”. alisisitiza 

Amesema wanafunzi wengi wanakosa fursa ya vitendea kazi kama madaftari na kalamu hivyo ni jambo la  msingi kwa wadau wa elimu kuendelea kusaidia watoto hao na kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutekeleza sera ya Elimu Bila Malipo.

Waziri Jafo pia alizindua mpango maalum wa kusaidia wanafunzi wenye uhitaji maalum ambao ameupa jina la “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.

Waziri Jafo amesema ujumbe huo unamhusu mtoto mwenye uhitaji wa kupata elimu na kuwaomba  Watanzania kwa ujumla kuunga mkono jambo hilo.

Amewaomba wadau hao wasichoke na wasikate tamaa kuchangia kwani watoto wengi wamepotea kwa kukosa vitedea kazi hivyo ni vyema kuwaokoa watoto hao na kuwatoa kwenye mazingira hatarishi. 

"Hivyo ni vyema watanzania kuwaunga mkono wadau wa elimu kwani wameongeza nguvu kazi kwa serikali kuwapatia elimu watoto wenye uhitaji,"amesema

Ameongeza "Japo kuna changamoto kubwa lakini ni vyema kujikita zaidi kusaidia Umma  na kuunga mkono kutatua changamoto za elimu,".

Amesema wengine ni yatima hawapati mahitaji maalum ya shule hivyo wakisaidiwa itakua ni jambo la muhimu sana. 

Amewashawishi Watanzania kushirikiana kwa pamoja kusaidia mpango huu ambao utawasaidia watoto wenye mahitaji maalum.

0 maoni:

Chapisha Maoni