Alhamisi, 1 Februari 2018

*RC MAKONDA AKOSHWA NA KASI YA UJENZI WA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA BAKWATA*

Posted by Esta Malibicheon Februari 1,2018 IN NEWS



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* leo amefanya *ziara* ya kukagua maendeleo ya *ujenzi* wa jengo la *Ofisi za Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA* ambapo amefurahishwa na *kasi ya ujenzi* huo.

Ujenzi wa jengo hilo la *kisasa* ni jitiada za *RC Makonda* kuthamini na !kuwapa *heshima* *Viongozi wa Dini* kwa kuhakikisha wanafanyakazi katika *mazingira mazuri* na yenye *hadhi* kutokana na *thamani na mchango* wao mkubwa katika jamii.

Jengo hilo la kisasa lenye *Gorofa Nne pamoja na Ground floor* lina Ofisi ya *Mufti wa Tanzania, Ofisi ya katibu, VIP room, kumbi za mikutano, Ofisi za wafanyakazi, ofisi za mshauri,Jiko,Vyoo, sehemu ya Kufanya Dua* pamoja sehemu ya Mapokezi.

*RC Makonda* amesema kazi wanayofanya *Viongozi wa Dini* ni kubwa hivyo tunapaswa kuthamini kwa kuwaweka *mazingira mazuri ya kufanya kazi*.

Aidha *RC Makonda* amesema shauku yake ni kuona *hadi mwezi wa Ramadhani jengo linakuwa limekamilika* na kuanza kutumika.

Aidha *RC Makonda* amewaomba Viongozi wa Dini kuendelea *kuliombea Amani Taifa* na viongozi wake.

Kwa upande wake *Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber* amemshukuru *RC Makonda* kwa kuwajengea jengo hilo na kusema katika *Miaka 50 BAKWATA haijawahi kuwa na jengo zuri na lakisasa Kama hilo* hivyo *RC Makonda* anaweka historia ya kwanza.

*Mufti* amesema jengo lililokuwepo lilikuwa likiwafanya *kuona hata haibu* hata kupokea ugeni wa *viongozi wa kislamu ulimwenguni.*

Katika ziara hiyo Viongizi wa Dini kwa pamoja wamemuombea *Dua RC Makonda* pamoja na *Rais Dr. John Magufuli* kwa kuwezesha kujengwa kwa *msikiti wa Mfalme wa Morocco* wenye uwezo wa kuchukuwa *watu 8,000* ampapo ujenzi unaendelea.

*MKUMBUKE MUNGU WAKO SIKU ZA UJANA WAKO, RC MAKONDA UONGOZI WAKO UMEACHA ALAMA KUBWA


*.

0 maoni:

Chapisha Maoni