Posted by Esta Malibiche on FEBRUARI 23,2018 IN NEWS
Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akizungumza jambo na Mbunge
wa Jimbo la Songwe Mhe Philiph Mulugo wakati wa mkutano na wachimbaji
wadogo uliofanyika katika kijiji na kata ya Saza, Wilaya na Mkoa wa
Songwe, jana 22 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Baadhi ya wachimbaji wadogo wakimsikiliza Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati
wa mkutano na wachimbaji wadogo uliofanyika katika kijiji na kata ya
Saza, Wilaya na Mkoa wa Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati
wa mkutano na wachimbaji wadogo uliofanyika katika kijiji na kata ya
Saza, Wilaya na Mkoa wa Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Songwe
Naibu
Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesifu juhudi za
mbunge wa Jimbo la Songwe Mhe Philiph Mulugo kutokana na uwajibikaji
mkubwa katika kuwasemea wananchi wa jimbo hilo hususani katika
kuimarisha uchumi wa wananchi kupitia sekta ya Madini.
Mhe
Biteko ametoa pongezi hizo kwa mbunge huyo wakati akihutubia mamia ya
wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika
Kijiji na Kata ya Saza akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake Mkoani
Songwe.
Naibu
waziri huyo alisema kuwa mbunge huyo amekuwa mstari wa mbele katika
kuwatetea wananchi wake hususani katika kuchochea shughuli za maendeleo
ili kuongeza ufanisi wa maendeleo endelevu ya mtu mmoja mmoja na jamii
kwa ujumla wake.
Pongezi
hizo zinajili wakati ambapo mbunge Mulugo amefanikiwa kutatua mgogoro
uliodumu kwa muda mrefu kati ya kikundi cha TUJIKOMBE na Kampuni ya
Bafex kwenye eneo la uchimbaji dhahabu la mlima Elizabeth.
Katika
kumaliza mgogoro huo kampuni ya Bafex imekubali kugharamia mradi
utakaochaguliwa na kikundi hicho kama fidia ya gharama walizozitumia
wachimbaji hao kuendeleza eneo hilo.
"Mheshimiwa
Mulugo wewe ni hazina ya Songwe, namuomba Mungu aendelee kukutunza
kwaajili ya watu hawa. Mimi nipo Bungeni muda wote wewe ajenda yako ni
watu wako na unafanya hivyo bila kuchoka. Kwakweli wewe ni NOMA" Alisema
Mhe. Biteko huku akishangiliwa na mamia ya wananchi waliohudhuria
mkutano huo.
Sambamba
na hayo pia amempongeza Mbunge huyo kwa ushirikiano mzuri baina yake na
serikali ya Wilaya pamoja na Chama Cha Mapinduzi jambo ambapo linaakisi
uwajibikaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.
Alisema
kuwa kilio hicho cha wananchi kimedumu kwa muda mrefu hivyo jukumu la
serikali ni kutatua kero za wananchi sio kuchochea migogoro.
0 maoni:
Chapisha Maoni