Na Esta Malibiche
Mufindi
JUMUIYA ya Umoja wa vijana ccm Mkoa wa Iringa imeadhimisha miaka 41 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM kwa kufanya usafi katika Hospital ya wilaya ya Mufindi, kuwaona na kuwafariji wagonjwa kwa kutoa vifaa mbalimbali Pamoja na kuchangia damu,ambapo zilipatikana unit 15.
Akizungumza na mtandao huu wa Habari,[KALI YA HABARI BLOG]Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Iringa, Kenani Kihongosi alisema kuwa Lengo la kuadhimisha miaka 41 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi kwa kuchangia damu ni kupunguza vifo vinavyokana na ukosefu wa Damu katika Hospital mara Mgonjwa anapohitajika kuongezewa Damu.
Kihongosi alisema kuwa hitaji la Damu salama katika Hospital ni kubwa,kutokana kuongezeka kwa wananchi wanaohitaji kuongezewa damu kuwa kubwa.
Alisema kutokana na mwammo mdogo wa wananchi wanaojitolea kuchangia damu,hivyo Hospital nyingi zimekuwa zikikabiliwa na uhaba wa damu salama,hivyo aliwataka watanzania kujitokeza kuchangia damu ili kupunguza wimbi kubwa la vifo vinavyotokana na ukosefu wa damu.
‘Hospital zetu zina kabiliwa na changamoto ya uhaba wa damu salama kutokana na ongezeko la watanzania hasa watoto akina mama wanaopoteza damu wakati wakujifungua,na majeruhi wanaotokana na ajali wapotaka kuongezewa damu lakini inashindikana kutokana na uhaba wa damu hivyo hupoteza maisha.
Tumeshuhudia matukio mengi ya ndugu zetu wakipoteza maisha yao kwa kukosa damau, na wengine wakifikishwa Hospitalini wanakosa hata chupa moja ya damu na hatimae kupoteza maisha,hivyo jukumu la kuchangia damu ni la kila mtanzania ili kupunguza wimbi hili la ukosefu wa damu katika Hospital zetu na hatimae kupunguza au kumaliza kabisa vifo vinavyotokana na ukosefu wa damu,kwa kuchangia damu tutakuwa tumewaokoa watanzania wenzetu’’Alisema Kihongosi na kuongeza kuwa
‘Sisi kama vijana tumaeamua tuadhimishe miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi kwa kuchangia damu ili tuweze kuokoa uhai wa watanzani’’Alisema Kihongosi.
Akizungumza katika Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi,Kenanai Kihongosi aliitaka Halmashauri kuhakikisha asilimia 5 ya vijana inyotokana na makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri inawafikia walengwa kwa wakati na si vinginevyo.
‘’Ninakuomba Mkurugenzi uwasimamie maafisa maendeleo wa wilaya wa hakikishe wanatoa Elimu kwa Vijana juu ya uundaji wa vikundi ili waweze kunufaika na mikopo hiyo.
Pia aliwataka watumishi wa kufanya kazi kwa weredi na bidii ili kuendana na kasi ya Seriakali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dakta John Magufuli
‘’Kwa mtumishi ambae anaona hwezi kuendana na kasi ya Serikali hii ya awamu ya tano ni bora akatupisha ili waachie wengine amabao watakuwa tayari kuendana na kasi hii’’Alisema Kihongosi.
Aidha Uvccm Mkoa wa Iringa kwa Pamoja wamempongeza Mh.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatumikia watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao,huku akitekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM,huku wakiwaomba watanzania waendelee kumuombea kila iitwapo leo.
Wakati huo huo wanachama wapatao 120 wapya waliojiunga na chama cha Mapinduzi katika maadhimisho hayo walikabdhiwa kadi na kuapishwa.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni