Posted by Esta Malibiche on Februari 23,2018 IN NEWS
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua
kinu cha kuchakata dhahabu mara baada ya kutembelea mgodi wa uchimbaji
dhahabu wa Shanta Gold Mine uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza akiwa
katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe, Leo 22 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua
baadhi ya mitambo ya uchenjuaji madini katika mgodi wa uchimbaji
dhahabu wa Shanta Gold Mine uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza akiwa
katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua
njia ya kwenda kwenye mgodi wa chini mara baada ya kutembelea mgodi wa
uchimbaji dhahabu wa Shanta Gold Mine uliopo katika Kijiji na Kata ya
Saza akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wafanyakazi wa mgodi wa Shanta uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza Wilayani Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Songwe
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesifu utendaji unaofanywa na
kampuni ya uchimbaji madini ya dhababu wa Shanta Gold Mine kwa kukubali
kuendana na matakwa ya serikali kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria
za nchi katika sekta hiyo.
Alisema
kuwa Wizara hiyo imedhamiria kuboresha sekta ya Madini ili wananchi
waweze kunufaika na rasilimali hiyo ambayo imechezewa na wajanja
wachache katika kipindi cha muda mrefu.
Mhe
Naibu Waziri huyo ametoa kauli hiyo Leo 22 Februari 2018 wakati
akizungumza na wafanyakazi wa mgodi wa Shanta uliopo katika Kijiji na
Kata ya Saza Wilayani Songwe.
Kampuni
ya SGM haipo kwenye kundi la wawekezaji walalamikaji kuwa serikali
kupitia sheria ya madini inawakimbiza wawekezaji jambo ambapo sio kweli
badala yake serikali imeweka utaratibu yakinifu wa uchumi fungamanishi
utakaoboresha sekta ya Madini na kuwanufaisha watanzania.
"Twendeni
kwa watanzania tukawaulize wamenufaika kwa kiasi gani na uwepo wa
migodi mbalimbali ya uchimbaji nchini, jibu ni jepesi tu kuna watu
wachache wamenufaika na rasilimali hiyo jambo ambapo hatutalifumbia
macho tena" Alisema Mhe Biteko na kuongeza kuwa
"Serikali
inahitaji wawekezaji ambao wanafuata sheria Na taratibu za nchi hata
kama ni wachache wanapaswa kufahamu kuwa wanapaswa kufuata sheria kwani
kufanya hivyo sio ombi bali ni lazima"
Aliongeza
kuwa Wizara ya Madini itaendeleza ushirikiano kwa kiasi kikubwa na
mgodi huo ili kuinua zaidi uwekezaji wao na hatimaye kuwa na uzalishaji
wenye tija ambao utapelekea serikali kukusanya kodi kwa kiasi kikubwa
kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla wake.
Alisema
kuwa watumishi wote katika Wizara ya Madini na wawekezaji katika sekta
ya madini wanapaswa kusimamia haki katika utendaji wao huku wakiunga
mkono juhudi za serikali katika kuimarisha nidhamu ya uwajibikaji
hususani kujitenga na utoaji ama upokeaji wa rushwa.
Alisema
dhamira ya serikali ya awamu ya tano ni kuwarahisishia huduma
wachimbaji wadogo kupitia malezi bora ya Wizara ya madini ili kufikia
hatua ya kuwa wachimbaji wa kati na hatimaye kufikia uwekezaji mkubwa
katika uchimbaji wa rasilimali hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni