Jumatatu, 26 Februari 2018

WATOTO 6 WAWASHIWA VIFAA VYA USIKIVU (COCHLEAR IMPLANT)

Posted by Esta Malibiche on februari 26,2018

0001
Mtaalam wa Huduma ya Usikivu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Mathayo Majogoro Alfred (katikati) akiunganisha kifaa cha usikivu cha nje na cha ndani ili mtoto Matilda Katobesi aweze kusikia kwa mara ya kwanza. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Pua, Koo na Masikio, Dkt. Edwin Liyombo akifuatilia na kushoto ni mama wa mtoto huyo, Angelina Cosmas.
0002
Mtoto Matilda kwa mara ya kwanza leo tarehe 24, Januari, 2018 akianza kutamka baadhi ya maneno baada ya kufundishwa na mtaalamu wa sauti kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili.
0003
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Pua, Koo na Masikio, Dkt. Edwin Liyombo wa Muhimbili akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuwasha kwa mara ya kwanza vifaa vya usikivu kwa watoto waliofanyiwa upasuaji na kupandikizwa vifaa hivyo katika hospitaili hiyo. Kuanzia kushoto ni Mkuu wa Idara ya Macho, Dkt. Baruani, Katibu wa Umoja wa Watoto na Wazazi Wanaonufaika na Vifaa vya Usikivu nchini, Bupe Mwakalambile na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Wateja, Bwana Aminiel Aligaesha.
????????????????????????????????????
Wazazi wakisubiri kuashwa kwa mara ya kwanza kwa vifaa vya usikivu katika hospitali hiyo.
0005
Mtaalamu wa Sauti, Fayaz Jaffer akionyesha kifaa cha usikivu (Cochlear Implant) kwa waandishi wa habari ambacho kinapandikizwa kwa mtoto mwenye tatizo la kusikia. Kulia ni Paul Khalil kutoka Kampuni ya Medel. Kuanzia kushoto ni Dkt. Edwin Liyombo, Dkt. Baruani, Bi. Bupe Mwakalambile na  Bwana Aminiel Aligaesha wakiwa kwenye mkutano huo leo.
????????????????????????????????????
Wazazi wa watoto wenye matatizo ya kusikia wakiwa kweny mkutano huo leo.
PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

………………..

Dar es salaam                                                                                           
Watoto sita ambao wamewekewa vifaa vya usikivu Januari mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo wameanza kusikia kwa mara ya kwanza baada ya kuwashiwa vifaa hivyo.
Kuwashwa kwa vifaa hivyo kumeleta furaha kwa wazazi kwani wameshuhudia watoto wao wakisikia sauti kwa mara ya kwanza na hivyo kuwajengea matumaini ya watoto hao kuanza maisha mapya.
Zoezi la kuwawashia vifaa hivyo (Switch On) limefanyika leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili  kwa kushirikiana na wataalaam kutoka Medel Austria ambao ndio wasambazaji wa vifaa hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari , Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Pua,  Koo na Masikio Dkt. Edwin Liyombo amesema watoto hao walifanyiwa upasuaji wa upandikizaji kifaa cha usikivu Januari mwaka huu ambapo zaidi ya asilimia 80 ya upasuaji huo ulifanywa na watalaam wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .
 ‘’Watoto hawa wataanza maisha mapya ya kusikia sauti mbalimbali katika mazingira yanayowazunguka baada ya kuunganisha vifaa hivi na kuviwasha’’. Amesema Dkt. Liyombo
Akifafanua amesema mbali na watoto hao sita lakini pia watoto wengine watano ambao walifanyiwa upasuaji huo mwaka jana  na  wengine sita  ambao walifanyiwa upasuaji huo nchini India nao wamekuja kufuatiliwa maendeleo yao ili kubaini changamoto zinazowakabili  na kupewa ushauri wa kitaalam. 
Akielezea ukubwa tatizo  Dkt. Liyombo amesema takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinaonesha kuwa katika watoto 1,000 wanaozaliwa,  inakadiriwa kuwa watoto watano wanazaliwa na tatizo kubwa la usikivu .
Pia amesema MNH ipo kwenye mchakato wa kuanzisha utaratibu wa kuwachunguza watoto wachanga ili kubaini mapema wenye matatizo yakutosikia.
Kwa upande wake Muwakilishi kutoka Medel Fayaz Jafar amesema upasuji huo umekua na mafanikio makubwa kwakua  katika awamu hiyo kumekua na mabadiliko  kwani asilimia kubwa  ya upasuaji umefanywa na watalaam wa MNH  na kwamba hatua hiyo ni ya kuridhisha.
Huduma ya Upandikizaji wa kifaa cha usikivu (Cochlear Implant) ilizinduliwa Juni 7 , 2017 na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu hivyo Tanzania imekuwa nchi ya pili kutoa huduma hiyo katika nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Kenya. Aidha Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutoa huduma hiyo  kupitia Hospitali ya Umma ambayo ni Muhimbili yenye hadhi ya ubingwa wa hali ya juu.

0 maoni:

Chapisha Maoni