Jumapili, 4 Februari 2018

SALIM ASAS:CCM HAITAMVUMILIA MTUMISHI YEYOTE WA SERIKALI ATAKAE KWAMISHA JUHUDI ZA MH.RAIS MAGUFULI


Posted by Esta Malibiiche ON FEBRUARI 5,2018 IN SIASA

.MNEC wa Mkoa wa Iringa,ambae pia ni  mjumbe wa Halmashauri kuu  CCM Taifa Salim Abri Asas,akizungumza na wanachama cha Mapinduzi,wakati wa maadhimisho ya miaka 41  ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM

Na Esta Malibiche
Iringa
NEC wa Mkoa wa Iringa,ambae pia ni  mjumbe wa Halmashauri kuu  CCM Taifa Salim Abri Asas amewataka watendaji wa umma  kuhakikisha wanatekeleza Irani ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo kwa kutokwamisha juhudi za Serikali .
Hayo ameyasema wakati wa maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mpinduzi CCM Mkoa wa Iringa,ambapo alisema kuwa hawatamfumbia macho mtu yeyote atakaethbutu kukwamisha miradi ya maendeleo kwa makusudi  mazima,tunataka wananchi wetu waendelee kuimani ccm kwa kupata maendeleo yanayotokana na Serikali ya ccm.

Sisi kama Chama Cha Mapinduzi hatutakubali kuona juhudi za Mh.Rais zinakwamishwa na mtu Yeyotena atakaethubutu tutapambana nae,sababu Serikali hii ya Dakta Magufuli imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananachi na wanyonge,hivyo kila mtumishi wa umma anapaswa afanye kazi kwa weredi’Alisema Asas.
Awali katibu wa chama cha MAPINDUZI ccm Mkoa wa Iringa, Christopher Magala akimkaribisha Mgeni rasmi alisema kuwaaliwata aliwata watendaji wa serikali na taasisi zake kuwa  watekerezaji wa sera na maamuzi ya chama tawala kwani ndiyo chama kilichochaguliwa na wananchi.
 Magala alisema kuwa Chama cha Mapinduzi hakitamvumilia mtendaji yeyote wa serikali au kiongozi  anayetaka kukwamisha sera na maamuzi ya CCM bali wawe mstali wa mbele katika kutatua kero za watu na si wao kuwa sehemu ya kero kwa wananchi wao wanaowategemea .

 ''Watendaji hao wanatakiwa kuhakikisha wanangaile na shida za wananchi  kwani hivi sasa kumekuwa viongozi wa serikali ndiyo wamekuwa kero kwa wananchi kwa kuwasumbuasumbua mara kwa mara  bila hata kuwapa elimu kwanza wananchi kabla ya kuwavunjia au kukamata vifaa vyao aambavyo ndiyo vinawaingizia kipato''Alisema

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na wanachama cha Mapinduzi,wakati wa maadhimisho ya miaka 41  ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM.





Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na wanachama cha Mapinduzi,wakati wa maadhimisho ya miaka 41  ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM.

 Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Iringa  mjini,Said Rubey akizungumzana wanachama cha Mapinduzi,wakati wa maadhimisho ya miaka 41  ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM.









0 maoni:

Chapisha Maoni