Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu akisalimiana na Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza mara bada ya kuwasili Mkoani Iringa,katika kijiji cha Kising'a kilichopo kata ya Kisinga'a Tarafa ya Isimani,Halmashauri ya wilaya ya Iringa Vijijini Mkoani Iringa.
Na Esta Malibiche
Iringa
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo hii amezindua Zahanati katika kijiji cha Kiding'a kilichopo Tarafa ya Isiman Halmashauri ya Iringa Vijijini Mkoani Iringa.
Akizungumza na wananchi wa Iringa katika hafla fupi ya uzinduzi wa Zahanati hiyo,Mama Samia Suluhu Hassan aliwapongeza wadau wa Maendeleo ambao ni kampuni ya Asas group kwa kuchangia kiasi cha Mill 125 na wananachi ambaoa walichangia kiasi cha Mill 4,higyo kufikia jumla ya Mill 129 na hatimae ujenzi ukakamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi,ambapo inahudumia vijiji vitatu na kaya 129 zinanufaika na mataibabu.
Alisema kuwa kutokana na juhudi kubwa iliyofanywa na wadau wa maendele kwa kushirikiana na wananchi Serikali kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo itahakikisha zahanati hiyo inapanuliwa na kuwa kituo cha Afya ili
kiweze kuhudumia wananchi wengi zaidi hivyo kupunguza Msongamamno katika Hospital ya wilaya na Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
“
"Ninawaomba wananchi tuendelee kushirikiana kuchangia ili wodi nzima ya akina mama .Pia tunawashukuru wananchi kwa kupisha ujenzi wa wodi hizi mbili ya wanaume na wanawake,kilichobaki tushirikiane kea pamoja kuhakikisha tunaongeza wodi nzima ya akina mama ikiwa ninpamoja na kuipanua kiwe kituo cha Afya"Alisema Mama Samia
Aidha Makamu wa Rais alikagua upanuzi wa kiwanda cha Ivory kilichopo katika Eneo la Ipogolo Manispaa ya Iringa,na kuipongeza Kampuni ya Ivory kwa kuboresha kiwanda hicho na kuunga mkonomjuhudi za Serikali.Pia alipongeza kwa kutoa ajira kwa vijana wapatao 150
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Iringa,aliomba Serikali kupitia Makamu wa Rais kuwasaidia wananchi wa Kising'a ususani kata Tarafa ya Isimani kutatua kero ya Maji iliyodumu kwa muda mrefu bila kutatuliwa, hasa vijiji vya pembezoni.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa Zahanati kwa Mh.Makamu wa Rais,Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Vijijini,alisema kuwa zahanati hiyo itahudumia wananchi wa vijiji 3,ambavyo ni Kising'a,Kinywang'anga na Igingilanyi pia jumla ya wananachi wapatao13672,wakiwamo wanaume 1943 na wanawake 229 watanufaika na matibabu katika Zahanati hiyo,ambayo inahudumiwa na wahudumu 4.
Aidha aliishukuru Kampuni ya Asas group kwa kujitoa katika Sekta ya Afya na kiboresha Afya za wananachi wa Kising'a na kuwataka wadau wa maendeleo wilayani humo,kujitolea katika sekta mbalimbali na si kuiachia Serikali pekee.
Akizungumzia hali ya upatikananji wa matibabu ndani ya Halmashauri hiyo alisema kuwa Halmashauri hiyo inavituo vya kutolea huduma ya Afya 76,ambapo kati ya hivyo vituo 65 ni Zahanati,vituo vya Afya 10 pamoja na Hospital ya wilaya 1.
"Mheshimiwa Makamu wa Rais kati ya vituo hivi,vituo 61 vinamilikiwa na Serikali na vituo..vinamilikiwa na Taasisi za mashirika ya dini na taasisi binafsi ni 15.Pia huduma za Afya ya uzazi na mtoto zinaendelea vizuri pamoja na huduma za wajawazito na huduma za kuondoa maabukizi ya vvu zinatolewa katika vituo vyote 72"" Alisema.
Aliongeza kuwa kuna pamoja na mafanikio hayo lakini wanakabiliwa na changamoto ya uzio zunguka zahanati hiyo na pamoja na fedha kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi waliopisha eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya.
Makamu wa Rais anaendelea na ziara yake Mkoani hapa,ambapo kesho Februari 10 atakagua miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Kilolo.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni