Posted by Esta Malibiche on FEBRUARI 1,2018 IN SIASA
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Iringa Nikolina Lulandala akimkabidhi vifaa tiba Ofisa muuguzi msaidizi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa Bi. Victory Ntara leo hii .
Na Esta Malibiche
Iringa
UWT Mkoa wa Iringa umeadhimisha miaka 41 ya kuzaliwa kwa
Chama cha Mapinduzi CCM kwa kutoa Msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh. 8.3
.katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Iringa, na kutembelea Wodi ya wagonjwa na kuwafarij.
Akizungumza wakati
wa kukabidhi vifaa hivyo, Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa, Nikolina
Lulandala alisema kuwa lengo la kutoa vifa hvyo ni kupunmguza
changamoto inayoikabili sekta ya Afya hasa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa
Lulandala alisema kuwa walifanya
utafiti kwanza kabla ya kununua vifaa tiba ambavyo wamevitoa msaada ili kuweza
kutatua changamoto kwenye maeneo ambayo ndio yanakumbana na changamoto husika.
“Tumeamua kufanya hivi kwa lengo la kuboresha
sekta ya afya kwa kuwa tumegundua kuwa hapa kuna changamoto nyingi hivyo sisi kama wanawake ndio maana tumeamua kutafuta wadau watusaidie kwa kuokoa maisha ya
wagonjwa wanaokuja kutibiwa hapa” alisema Lulandala
Aidha vifaa tiba ambavyo wamekabidhi
hospitalini hapo nipamoja na Injection Gentramicin, boksi 1000, Nabulaiza
1, Injection Ampiliciline vipande 1000,Suction Mashine 2, box za sabuni, mafuta
ya kupaka watoto na biskuti.
Alisema kuwa anaishukuru serikali ya
awamu ya tano kwa kufanya kazi kwa kuwafikia wananchi wa chini hasa wale
wanyonge kwa kutimiza kile ambacho kilikuwa kimeahidiwa wakati wa kuomba kura
za kuongoza nchi.
Lulandala alisema kuwa serikali ya
awamu ya tano imefanikisha kuleta mabadiliko ya haraka katika sekta ya afya
tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea
kufanya kazi kwa kujituma ili kuunga mkono juhudi hizi.
“Najua kuwa mnaona kwa macho yenu
kiasi gani serikali ya wamu ya tano jinsi gani huduma za afya zilivyo boreshwa
na lazima tujivunie hiki kinachofanywa na Rais wetu,mimi binafsi naunga mkono
juhudi hizi na ninaomba wananchi nao waunge mkono juhudi hizi” alisema
lulandala
Lulandala aliongeza kuwa kuongezaka
kwa hospital za rufaa kwenye mikoa,vituo vya afya kwenye kata au tarafa,
zahanati kwenye vijiji na mitaa ni hatua kubwa ya kimaendeleo hivyo ndio
serikali ya awamu hii inavyotekeleza vilivyo ilani ya chama cha mapinduzi ya
mwaka 2015 hadi 2020.
Lakini sio afya tu hata ukiangalia
saizi tunapata elimu bure ambayo inamwezesha kila mwanafunzi kusoma bure na
kuhakikisha tunapunguza wimbi la wanafunzi kukosa elimu ambapo inasaidia kuwa
nakizazi cha wasomi hapo baadae.
Kwa upande wake Ofisa muuguzi
msaidizi wa Hospital Rufaa ya Mkoa wa Iringa hiyo Victory Ntara aliwashukuru UWT kwa kutoa vifaa hivyo vya tiba na kuwataka
wadau mbalimbali waeweze kuiga mfano huo na hatimae chamngamoto mbalimbali za
ukosefu wa vifaa tiba katika Hospitali hiyo iweze kumalizika.
“Tunaomba mtufikishe salamu kwa Rais
wa serikali ya awamu ya tano kwa kazi kubwa anayoifanya kwa kuboresha sekta ya
afya kwa kuwa hali ya sasa kila kitu kinaenda kwa wakati” alisema Ntara
Mwenyekiti UWT Mkoa wa Iringa Nikolina Lulandala akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa tiba kwa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa leo hii.
Katibu wa UWT Mkoa wa Iringa Chiku Masanja akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa tiba kwa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa leo |
Mwenyekiti UWT Mkoa wa Iringa Nikolina Lulandala akimkabidhi vifaa tiba Ofisa muuguzi msaidizi wa hospital wa Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
Uwt wakiendelea kukabidhi ifaa tiba
Uwt wakiendelea kukabidhi ifaa tiba
Uwt wakiendelea kukabidhi ifaa tiba
Uwt wakiendelea kukabidhi ifaa tiba
Uwt iwakiendelea kukabidhi ifaa tiba
Vifaa mbalimbali vilivyokabidhiwa na UWT Mkoa wa Iringa,kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa mapema leo hii
Vifaa mbalimbali vilivyokabidhiwa na UWT Mkoa wa Iringa,kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa mapema leo hii
0 maoni:
Chapisha Maoni