Posted by Esta Malibiche on FEBRUARI 8,2018 IN NEWS
Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Amina Msenza akizungumza ofisini kakwe na vyombo vya Habari mapema leo hii,kuhusu ujui wa Makamu wa Rais,anaetarajia kuaNza ziara ya kikazi kesho Mkoani Iringa.PICHA NA ESTA MALIBICHE.
Na Esta
Malibiche
Iringa
Mkuu wa Mkoa
wa Iringa Amina Masenza amewataka
wananchi wa Mkoa wa Iringa, Kujitokweza kawa wingi kumpokea Mkamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan anaetarajias
kuanza ziara ya kikazi hapo kesho.
.
Mapokezi
hayo yatafanyika kwenye kijiji cha
Kising’a wilaya ya Iringa kuanzia saa 3;00 asubuhi.
Akizungumza
ofisioni kwake na Vyombo vya Habari
mapema leo hii, alisema kuwa makamu wa Rais atafanya ziara ya kikazi Mkaoani
hapa kuanzia kesho tarehe 9,2,2018 na
kuhitimisha tarehe 13,2,2018.
Masenza alisema
katika ziara hiyo Makamu wa Rais anatarajia kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa mkoani Iringa na
Serikali na Sekata binafsi,vilevile atafanya mikutano ya hadhara.
‘’Ndugu wananchi
wa Mkoa wa Iringa,tarehe 9,2,2018 Mheshimiwa Makamu wa Rais atapokelewa katika Halmashauri ya
Iringa,ambapo atafungua wodi katika
zahanati ya kijiji cha Kisinga’a,atakagua
upanuzi wa kiwanda cha Ivory,atakagua kiwanda cha Ufungashaji wa mazao ya Mbogamboga
,pia atafungua barabara ya mashine tatu’’alisema Masenza ana kuongeza kuwa
‘Tarehe
10,2,2018 Mheshimiwa makamu wa Rais
ataelekea wialaya ya Kilolo ambapo atazindua jengo la utawala katika
Shule ya Sekondari Kilolo na atafanya Mkutano wa hadhara kwenye mji mdogo wa
Ilula.
Alisema kuwa
Tarehe 11,2,2018 atakuwa wilayani Mufindi ambako ataweka jiwe la Msingi maabara kwenye Shule ya Sekondari
Mgololo,atafungua Zahanati ya kijiji cha Mtili na kukagua kiwanda cha
utengenezaji wa Mkaa Mafinga.
Masenza
aliongeza kuwa tarehe 12,2,2018 Mheshimiwa makamu wa Rais atazindua Mradi
wa kuendeleza utalii ukanda wa Kusini[REGROW] ambapo Mkoa wa Iringa ni kitovu cha
Utalii,ambapo uzinduzi huo utafanyika eneo la kihesa Kilolo Kuanzia saa 2;30 asubuhi na sa 8;00 Mchana atafanya
Mkutano wa hadhara katika uwanja wa mwembetogwa Manispaa ya Iringa.
‘’Ninawaomba
wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi
na Mkutano wa hadhara ili kwa Pamoja tupate kupokea ujumbe kutoka kwa
Mheshimiwa makamu wa Rais’’Alisisitriza Masenza
0 maoni:
Chapisha Maoni