Posted by Esta Malibiche on Fbruari 26,2018
Wahamiaji haramu waliokamatwa Iringa |
WAHAMIAJI haramu 83 wamekamatwa na idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Iringa jana huku baadhi yao wakiwa katika hali mbaya baada ya kukosa chakula siku tatu.
Akizungumza mara baada ya kuwafikisha katika kituo cha Polisi mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Mkoa wa Iringa, Hope Kawawa ,alisema wahamiaji hao walikamatwa katika maeneo ya kijiji cha Mbigili wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wakiwa katika roli aina ya Scania baada ya kupata taarifa kutoka raia wema.
Kawawa alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo walifanikiwa kulikamata roli hilo lenye namba T903 AKH mali ya Gabriel Mwakyambiki mwenyeji wa Tukuyu ambapo dereva alifanikiwa kukimbia na kulitekeleza roli hilo kijiji cha Mbigili.
Alisema wahamiaji hao walikamatwa majira ya saa kumi na moja juzi jioni na maafisa wa uhamiaji kwa kushirikiana na jeshi la polisi hivyo wakiwa katika hali mbaya ambapo wengi wao walionekana wakiwa hawajapata chakula hali iliyolazimu kuwapatia kwanza huduma ya kwanza hadi hali zao zitakapotengemaa.
Alisema Kawawa alisema kuwa baada ya wiki iliyopita kuwakamata wahamiaji wanne waliendelea kufanya doria na kufanikiwa kuwakamata wahamiaji 83 juzi ambao watawafikisha mahakamani mara baada ya hali zao kuwa njema.
Aidha alitoa wito kwa wanaofanya biashara ya kuwasafirisha wahamiaji hao kuwa kwa sasa mkoa wa Iringa si mahala pa kupitisha wahamiaji bali wataendelea kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wahamiaji wote watakaogundulika mkoani hapo na wako kazini kwa masaa ishirini nne.
“Naomba niwaambie madalali wanaosafirisha hawa wahamiaji mkoa wa Iringa sio mahala salama kabisa kuwapitisha hao watu kwani tuko makini masaa 24 na pindi tukiwabaini hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa kufanya biashara ya kuwasafirisha wahamiaji hivyo wasitarajie watapita mkoa wa Iringa bila kuwakamata” alisema
Kawawa alitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na idara ya uhamiaji kwa kutoa taarifa pindi wanapohisi baadhi ya watu sio raia wa Tanzania na watu wasiowajua kwenye vyombo vya usalama ili wachunguzwe na kuchukuliwa hatua madhubuti.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinza na usalama mkoa wa Iringa akizuingumza baada ya kuwatembelea wahamiaji hao ambao baadhi yao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa alisema kuwa mkoa wa Iringa umejipanga kiusalama na kuwa si rahisi kwa wahamiaji kuvuka ndani ya mkoa huo .
wahamiaji haramu raia wa Ephiopia wanaswa Iringa wakisafirishwa kwenye Lori
Wahamiaji hao wakiwa hoi
0 maoni:
Chapisha Maoni