Jumatatu, 26 Februari 2018

MAVUNDE AAGIZA WAAJIRI MWANZA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSHINDWA KUJISAJILI MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI-WCF

Posted by Esta Malibiche on Februari 26,2018 IN NEWS

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde ameagiza Wakurugenzi wa Kampuni ya  Ujenzi ya *JASCO LTD,AIRCO na JB BELLMONT HOTEL* kufikishwa Mahakamani kwa kushindwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF).

Mavunde ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake katika mkoa wa Mwanza kukagua Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa Agizo la *Mh* *Waziri Jennister Mhagama* ambaye aliwataka waajiri wote nchini wawe wamejisajili kwenye mfuko wa Fidia wa Wafanyakazi kabla au ifikapo tarehe *30.09.2017*

Katika Mkoa wa Mwanza jumla ya waajiri takribani 700 hawajajisajili katika mfuko wa Fidia wa Wafanyakazi ambapo zoezi la msako wa waajiri hao litaendelea kwa wiki nzima na kuwachukulia hatua stahiki wale waajiri wote wataokuwa hawatii matakwa ya sheria ya Fidia ya Wafanyakazi.

Kwa mujibu wa Kifungu cha  71(4) Mwajiri yoyote atakayeshindwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi atashitakiwa Mahakamani na akikutwa na hatia adhabu yake ni faini isiyozidi *TSh* *50,000,000* au kifungo cha *miaka mitano* au vyote kwa pamoja.

Aidha Mavunde amemuagiza Afisa Kazi Mfawidhi wa Mwanza kuwapa waajiri hao Amri tekelezi ya siku 30 kutekeleza matakwa ya Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Na. 6/2004 kwa kuwapa Wafanyakazi wao mikataba,malipo ya mshahara kwa kima cha chini cha sekta husika na kuwasilisha michango ya wafanyakazi katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.












0 maoni:

Chapisha Maoni