Posted by Esta Malibiche on FEBRUARI 9,2018 IN NEWS
Na,Joel Maduka ,Nyang'hwale
Kampuni
ya uchimbaji madini ya dhahabu Acacia kupitia mgodi wake wa
Bulyanhulu imekabidhi hundi ya shilingi milioni 75,649,524 kwa
halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita kwa ajili ya malipo ya
ushuru wa huduma kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Disemba mwaka 2017.
Akikabidhi mfano wa hundi hiyo mbele ya madiwani wa halmashauri hiyo Meneja wa Mgodi huo, Benedict Busunzu, alisema kawaida mgodi huo hutoa ushuru kwa Wilaya mbili ya Msalala na Nyangh’hwale kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Aidha
alitaja moja ya miradi mingine ambayo mgodi huo umesaidia
Wilayani humo ni pamoja na mradi wa mkubwa wa kusambaza maji
kwa wakazi 150,000 wilayani humo, wenye gharama ya Shilingi
Bilioni 4.5 ambao unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Aidha
kwa upande wake Katibu tawala wa Mkoa wa Geita, Celestine Gesimba
amewataka madiwani na watendaji wa halmashauri ya hiyo kuepuka
kutumia fedha zinazotolewa na wadau mbali mbali kwa ajili ya
miradi ya maendeleo kwa kulipana posho za vikao, badala yake
zote zitumike katika miradi kwa manufaa ya ustawi wa wakazi wa
Wilaya hiyo.
“Ninapenda
kuwaonya viongozi na watendaji ambao mpo hapa Nyangh’wale kuwa
tusitumie hizi fedha kwa ajili ya kulipana posho za vikao
badala yake zote zietumike katika miradi ya maendeleo kwa
jinsi mtakavyoainisha,”alisema Gesimba.
Aidha Mkurugenzi wa Wilaya ya hiyo, Carlos Gwamagobe, pamoja na
kushukuru mgodi mgodi huo kwa kuwapatia fedha hizo alisema ushuru
wa huduma ambayo walikuwa wakipata hapo awali umeshuka kwani kwa kiasi
kikubwa kwani walikuwa wakipokea milioni mia nne kwa miezi sita .
“Tuna
imani kuwa mgodi huu ukianza shughuli zake kama ilivyokuwa
awali hata ushuru wa huduma utaongezeka kwani awali tulikuwa
tukipatiwa kiasi cha Shilingi Milioni 225 lakini tangu kuibuka
kwa sakata la Makinikia, ushuru nao umepungua mara mbili ya
zile za awali,”alisema Gwamagobe.
Meneja Mkuu wa Migodi wa Bulyanhulu Benedict Busunzu akifurahia pamoja na wafanyakazi wa Bulyanhulu baada ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale. |
0 maoni:
Chapisha Maoni