Jumatatu, 26 Februari 2018

MJUMBE WA BARAZA KUU TAIFA UVCCM GWANTWA MWAKIJUNGU AKABIDHI BATI 30 KATA YA KIJICHI

Posted by Esta Malibiche on Februari 26,2018 IN SIASA

 Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM,Mkoa wa -Dar es salaam Gwantwa Alex Mwakijungu amekabidhi bati 30 katika kata ya Kijichi kwa ajiri ya uezekaji wa ofisi ya serikali ya mtaa wa Mission iliyopo Kijichi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi alisema kuwa lengo la kutoa mchango huo ni kutaka kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Aidha aliwashuruku wakazi wa Kijichi kwa niaba ya Umoja wa Vijana CCM Dar es salaam kwa imani kubwa walionyesha kwa Chama Cha Mapinduzi na Vijana kwa kumchagua Mtalawanji kuwa Diwani wa kata hiyo katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.


"Mtalawanje ni Kijana mwenzetu. Kumchagua kwenu nyinyi wananchi wa Kijichi kuwa Diwani wenu ni dhamana ya vijana wote wa UVCCM Dar kwani yeye anatuwakilisha sisi. Utendaji wake ndio mwangaza wa sisi vijana katika duru za uongozi kwani akifanikiwa yeye,sisi tutakuwa na jeuri ya kugombea nafasi nyingine za uwakilishi kwa kumtumia yeye kama mfano wa kuwa Vijana tunaweza. Na nina waahidi kuwa sisi viongozi wa jumuiya tutakuwa nae bega kwa bega kuhakikisha mipango ya maendeleo ya Kijichi inafanikiwa" Alisema

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kijichi Mh Eliassa Kassim Mtalawanje alimshukuru  Alex kwa mchango wa bati pia aliwaomba wadau wengine mbalimbali waweze kujitokeza na kutia nguvu katika shughuli za kimaendeleo mbalimbali ili kusaidia kuonesha njia kwa serikali katika kutatua changamoto za wananchi.





0 maoni:

Chapisha Maoni