Jumanne, 13 Februari 2018

MAKAMU WA RAIS LEO AMEHITIMISHA ZIARA YAKE MKOANI IRINGA HUKU AKIZITAKA HALMASHAURI KUELEKEZA FEDHA KATIKA MIRADI YA MAENDELEO

Posted by Esta Malibche ON FEBRUARI 13,2018 IN KITAIFA



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao wakati wa majumuisho ya ziara yake mkoani Iringa, Wengine pichani ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza (kushoto)  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bw. Salim Abri Asas naWaziri wa Maliasili na utalii Hamis Kigwangala(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa mkoa wa Iringa kushirikiana ili kuweza Kuwasaidia wananchi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kutoa
majumuisho ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za
maendeleo mkoani Iringa.

Makamu wa Rais alitembelea wilaya ya Iringa, Kilolo na
Mufindi ambako kote alishiriki shughuli za kimaendeleo
ikiwa kuzindua Vituo vya Afya Kising’a wilaya Iringa, Jengo la Utawala na Madarasa katika Shule ya Sekondari Kilolo,
Pia aliweka jiwe la msingi katika Ujenzi wa Maabara na
Madarasa katika shule ya sekondari Mgololo na kuweka
jiwe la Msingi katika upanuzi wa Kituo cha Afya cha
Ihongole kilichopo Mafinga.

Makamu wa Rais pamoja na kutembelea miradi hiyo ya
kimaendeleo pia alitembelea Kiwanda cha Ivori
kinachotengeneza pipi na Chocolate na alitembelea
kampuni ya GBRI inayoshughulika na uzalishaji na uuzaji wa bidhaa za mboga mboga boga.

Katika ziara hiyo Makamu wa Rais amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Iringa kwa mapokezi mazuri waliompa katika kipindi chote cha Ziara yake .

Makamu wa Rais amesisitiza juu ya utunzaji wa Vyanzo vya Majina utunzaji wa Mazingira,ambapo amewataka viongozi wa Mkoa wa Iringa kuwa mstari wa mbele katika kutoa Elimu ya Mazingira na Elimu juu ya ugonjwa hatari wa Ukimwi ambao unaonekana kuenea kwa kasi kutokana na takwimu zake.

Aidha Makamu wa Rais aliwataka viongozi kuhakikisha wanatoa Elimu ya kutosha kwa wqnanchi juu ya umuhimu wa  kujiunga na mfuko wa Afya ili waweze kupata matibabu kwa nafuu.

Hata hivyo Makamu wa Rais alitoa Rai kwa viongozi wa Mkoa wa Iringa pamoja na wananachi kuunga mkono mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania (REGROW) aliouzindua jana,ambao utaweza kufungua faursa Mkoani Iringa  pamoja na  kutunza Mazingira.

Akihitimisha Makamu wa Rais ameahaidi kubeba Changamoto kubwa  zikiwemo barabara,Huduma za Afya,Elimu, Maji ambazo ni kilio kikubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa.



Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Alat Taifa,ambae pia ni Diwani   wa Kata ya Nzihi  kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Stephen Mhapa akimshukuru Makamu wa Rais kwa kutembelea Mkoa wa Iringa,aliiomba Serikali kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi  mbalimbali ya   mandeleo iliyoibuliwa na wananchi n kuwama kumaliza kutokana na kukosa fedha za kumalizia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Iringa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Iringa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Iringa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)







0 maoni:

Chapisha Maoni