Jumamosi, 3 Februari 2018

NAIBU WAZIRI MAVUNDE ASISITIZA ELIMU ZAIDI JUU YA TATIZO LA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA

Posted by Esta Malibiche ON FEBRauARI 3,2018 IN NEWS

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Peter Mavundeambae pia ni Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM,akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya ..Wasichana-Msalato,Dodoma wakati akihitimisha kampeni ya Elimu ya Tatizo la Usugu wa vimelea vya dawa 

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Peter Mavunde amesisitiza kuwepo kwa kampeni kubwa ya nchi nzima juu Elimu ya tatizo la Usugu wa vimelea vya dawa.

Mavunde ameyasema hayo leo wakati akihitimisha kampeni ya Elimu ya Tatizo la Usugu wa vimelea vya dawa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana-Msalato,Dodoma ambapo ametumia fursa hiyo kuwataka wadau na taasisi mbalimbali za umma na binafsi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Chama cha Wanafunzi Wafamasia Tanzania(TASPA) ambao wamejitolea kutembea nchi nzima kutoa elimu.

“Najua moja kati ya sababu nyingi zinazosababisha usugu wa vimelea vya madawa ni ubora hafifu wa dawa na utoaji wa dawa pasipo cheti cha daktari”Alisema Mavunde


Kufuatia hali hiyo Mavunde ametumia
nafasi hiyo kwa kuzitaka Taasisi za TFDA na BARAZA LA WAFAMASIA TANZANIA kuchukua hatua kali na stahiki kwa wale wote wanaovunja sheria na miongozo iliyowekwa katika kusimamia masuala yote ya dawa na tiba.


Akimkaribisha Mgeni Rasmi Rais wa TASPA ndg Erick Venant alieleza kwamba kampeni hiyo ya kujitolea wamefanya nchi nzima kwa mikoa 23 na Shule za Sekondari 123 na wamewafikia takriban watanzania 6 milioni.Ndg Venant aliendelea kusisitisa kwamba tatizo hili ni hatari kuliko hata ugonjwa wa UKIMWI kwa kuwa takribani watu 700,000 wanafariki kila mwaka kutokana na tatizo hilo na ikisiwa ifikapo 2050 jumla ya watu 10 milioni watakufa kwa mwaka.











0 maoni:

Chapisha Maoni