Posted by Esta Malibiche on februari 26.2018 in News
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza (watatu kushoto) akishangaa gari la Benki la NMB lenye ATM ikiwa na Benki ndani yake huku Huduma za kibenki zikiendelea katika stendi ya mabasi yaendao mikoani mjini IRINGA baada ya kuzindua tawi jipya la NMB Ruaha Ijumaa wiki iliyopita. (Picha na Friday Simbaya)
|
IRINGA:
Wakulima mkoani Iringa wametakiwa kuzitumia taasisi za kifedha mkoani humo kwa kuchukua mikopo nafuu ili kulima kilimo chenye tija na kukuza uchumi wao badala ya kulima kilimo cha mazoea hali inayopelekea kushuka kwa uchumi wao.
Imeelezwa kuwa moja ya sababu inayochangia wakulima wengi kushindwa kulima kilimo cha kitaalamu ni ukosefu wa mitaji hali inayopelekea kuendelea kulima kilimo kwa mazoea
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa iringa amina masenza hivi karibuni wakati akazindua tawi jipya la bank ya NMB Ruaha ambalo linatajwa kupunguza msongamano wa wateja huku akiwataka wananchi kuendelea kuzitumia taasisi hizo kwa kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.
Masenza alisema ili mkulima ajikwamue kiuchumi anapaswa kulima kilimo cha kisasa tofauti na ilivyozoeleka kwa wakulima wengi huku akizitaka taasisi za kifedha nchini kutoa kipaombele kwa wakulima.
upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Biashara NMB Abdulmajid Nsekea aliwataka wanawake na vijana ambao wapo katika vikundi vya ujasiliamali kuchangamkia fursa ya mikopo inalotolwa na benki hiyo.
Alisema uzinduzi wa tawi jipya la bank ya NMB Ruaha litakupunguza msongamano wa wateja katika benki ya Mkwawa, huku akiwataka wananchi kuendelea kuzitumia taasisi hizo kwa kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.
0 maoni:
Chapisha Maoni