Alhamisi, 22 Februari 2018

JAFO AWAPONGEZA VIONGOZI WA MKOA WA SINGIDA

Posted by Esta Malibiche on Februari 22,2018  IN NEWS

 Majengo mapya ya Kituo cha Afya Kintinku wilayani Manyoni yanayoendelea kujengwa.




 Viongozi wakifanya ukaguzi katika majengo yanayojengwa katika Kituo cha Afya Kintinku wilayani Manyoni.




Wananchi wa kijiji cha Kintinku wakicheza ngoma za asili wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo.




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Singida kwa usimamizi wa Miradi ya ujenzi wa vituo vya afya unaoendelea mkoani humo hivi sasa.

Waziri Jafo ametoa pongezi hizo alipotembelea kukagua ujenzi wa kituo cha afya Kintinku kilichopo wilayani Manyoni mkoani Singida. 

Waziri Jafo ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho serikali imepeleka sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu.

Amebainisha Mkoa wa Singida unaendelea ujenzi katika vituo saba ambapo kila eneo maendeleo ya ujenzi yanaenda vyema.


Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Manyoni mashariki Daniel Mtuka kwa juhudi zake za kuwahangaikiwa wananchi wa Jimbo hilo


0 maoni:

Chapisha Maoni