Posted by Esta Malibiche on FEBRUARI 3,218
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa,Christopher Magala akikabidhi mifuko ya saruji kwa Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela,wakiwemo viongozi Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.PICHA NA ESTA MALIBICHE.
Na Esta Malibiche
Iringa
CHAMA cha Mapinduzi CCM Mkoa
wa Iringa kimesherekea miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama cha hicho kwa
kuchangia shughuli za maendeleo katika sekta ya Elimu.
CCM Mkoa wa Iringa imekabidhi
mifuko ya saruji 500 na bati 300 kwa uongozi wa Halmashauri ya Manispaa
ya Iringa kwa lengo la kukarabati miundombinu ya shule zilizochakaaa,huku
ikiunga mkono juuhudi za Serikali ya awamu ya Tanao kwa vitendo.
Akizungumza na wananchi katika
Shule ya Sekondari ya Mawelewele iliyopo kata ya Mwangata Manispaa ya
Iringa,wakati akikabidhi bati 60 na mifukio ya Saruji 60,katibu wa Chama cha
Mapinduzi ccm Mkoa wa Iringa,Christopher Magala alisema kuwa chama cha
amapinduzi kwa kutambua umhimu wa Elimu na Changamoto zinazoikabili seta hiyo
wameona washerekee miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama hicho kwa kuiangalia sekta ya
Elimu ndani ya manispaa ya Iringa.
‘Tumeamua kusherekea kwa kumuunga
mkono Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM taifa,Rais Dakta John Magufuli kwa
vitendo kwa kukabidhi msaada huo ili Pamoja na kuwaonyesha wananchi waliotuweka
madarakani jinsi gani tunatekeleza Irani yetu kwa vitendo na si kwa mamneno
tu’’Alisema Magala.
'Katika Risala ya Shule inaonyesha
kuwa kuna upungufu wa walimu wa sayansi,ninawaomba walimu muwajengee wanafunzi
wapende kusoma masomo ya sayansi ili tuweze kuwapata walimu wa masomo ya
sayansi ili Taifa liweze kuondokana na uhaba wa walimu wa Sayansi'aliema Mgala na kuongeza kuwa
'Katika shule hii kuna kero ya vyumba vya madarasa,Hosteli za watoto wa
kike,Nyumba za walimu na Maabala,ninawaomba wananchi tuendelee kushirikiana
wote bila kuiachia serikali pekee'Alisema Mgala na kuongeaza kuwa
'Sisi kama chama cha amapinduzi kwa
kuonyesha njia leo tunaikabidhi Serikali vifaa hivi ili viweze kupunguza kero
ya miundombinu katika shule yetu hii na Shule za Manispaa.'
Aidha Katibu wa Chama cha Mapinduzi
ccm Mkoa wa Iringa,aliwaongoza wanaccm kuchimba Msingi wa ujenzi wa vyumba vya
amadarasa katika eneo la shule ya Sekondari ya Mawelewele.Viongozi hao
walioshiriki nipamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela,Mkuu wa
Wilaya ya Mufindi Jmahuri David Willium,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa
Mjini,Iringa Vijiji,Kilolo na Mufindi.Pia wengine walioshiriki kuchimba Msingi
nipamoja na Katibu wa chama cha Mapinduzi ccm Iringa Mjini,Kilolo na Mufindi
pamoja na viongozi wa uvccm Mkoa wa Iringa na wilaya zote za mkoa wa
Iringa,wanachama na viongozi wa jumuiya za Chama cha Mapinduzi.
Akipokea Msaada huo,Mkuu wa wilaya
ya Iringa,Richard Kasesela alikishukuru
chama cha Mapinduzi kwa majitoleo yao na kusema kuwa vifaa hivyo vitaweza kukarabati
vyumba vya madarasa viwili vinavyotarajia kujengwa ambapo Msingi wakeuliozinduliwa
kuchimbwa na Chama cha Mpinduzi ccm.
Kasesela aliwataka wadau wa
amaendeleo wengine kujitolea ili waweze kukamilisha vyumba vya madarasa
vinavyoendelea kujengwa katika shule ya Sekondari ya mawelewele pamoja na
kuboresha miundombinu ya shule zilizopo
Mnispaa ya Iringa.
Tunakishukuru Chama cha Mapinduzi
kwa kuona umuhimu wa Eliimu kwa vijana wetu na hatimae mmeweza kuchangia vifaa
hivi vitakavyoweza kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa uweze
kukamilika,ninawaomba na wadau wengine wa maendeleo wajitikeze kuchangia’’Alisema
Kasesela na kuongeza kuwa
“Halmashauri ya manispaa ya Iringa ni yatima
hivyo tunaomba chama cha mapinduzi kupitia viongozi wangu mtusaidie kufanya
shughuli za kimaendeleo msiishie leo tu maanakuna vitu vingi bado havijakaa
sawa” alisema Kasesela
Pia Kasesela alitoa agizo kwa mkuu
wa Shule kuhakikisha masaada huo uliotolewa na Chama cha Mapinduzi utatumika
kama ilivyopangwa na kuongeza kuwa kwa kiongozi yeyote atakae diriki kufanya ubadhirifu hatua
za kinidhamu zitachulkuliwa dhidi yake.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa,Christopher Magala akikabidhi mifuko ya saruji kwa Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela,wakiwemo viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa. |
Mifuko 60ya saruji iliyokabidhiwa katika Shule ya Sekondari ya Mawelewele ikiwa ni miongoni mwa mifuko 500 iliyokabidhiwa Halmashauri ya Manispaa ya IRINGA |
Mifuko 60ya saruji iliyokabidhiwa katika Shule ya Sekondari ya Mawelewele ikiwa ni miongoni mwa mifuko 500 iliyokabidhiwa Halmashauri ya Manispaa ya IRINGA |
Mifuko 60ya saruji iliyokabidhiwa katika Shule ya Sekondari ya Mawelewele ikiwa ni miongoni mwa mifuko 500 iliyokabidhiwa Halmashauri ya Manispaa ya IRINGA |
Katibu wa Chama cha Mapinduzi ccm Mkoa a Iringa,Christopher Magala akionyesha baadha i ya bati ambazo chama kimekabidhi kwa Shule ya Sekondari Mawelewele ikiwa ni miongoni mwa bati walizokabidhi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa,Richard Kasesela akichimba Msingi
wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Mawelewele
ikiwa ni moja ya kufanya kazi kwa vitendo
Mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa Said Rubeya akichimba Msingi
wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Mawelewele
ikiwa ni moja ya kufanya kazi kwa vitendo.
Mbunge waviti maalum mkoa wa Iringa kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Ritha Kabati akichimba Msingi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Mawelewele ikiwa ni moja ya kufanya kazi kwa vitendo.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana Mkoa wa Iringa Kenani kihongosiakichimba Msingi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Mawelewele ikiwa ni moja ya kufanya kazi kwa vitendo. |
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa,Christopher Magala akizundgumza na wananchi kijiji cha Mawelewele katika Shule ya Sekondari ya Mawelewele mara baada ya kuhitimisha zoezi la kufantya kazi kwa vitendo kwa kuchimba Msingi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa,Christopher Magala akizundgumza na wananchi kijiji cha Mawelewele katika Shule ya Sekondari ya Mawelewele mara baada ya kuhitimisha zoezi la kufantya kazi kwa vitendo kwa kuchimba Msingi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa,Christopher Magala akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa Shule ya Sekondari ya Mawelewele
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa,Christopher Magala akiwa katika picha yapamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mawelewele
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa,Christopher Magala
akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wanafunzi
0 maoni:
Chapisha Maoni