Posted by Esta Malibiche on februari 12,2018 in KITAIFA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla kabrasha lenye Andiko la mradi wa REGROW na Mikataba ya Fedha na utekelezaji wa mradi mara baada ya kuuzindua mradi huo katika eneo la Kihesa Kilolo mkoani Iringa.[PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS]
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imedhamiria kuleta
mabadiliko ya dhati katika sekta ya utalii kwa kuhakikisha inatanua mtandao wa
barabara na pia kuweka mikakati dhabiti ya kuviendeleza vivutio vya utalii
viliovyoko kanda ya Kusini ili vichangie
ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.
Makamu wa Rais aliyasema hayo leo kwenye
hafla ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii kanda ya kusini mwa Tanzania
uliofanyika Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
Makamu wa Rais alisema Serikali imeendelea
kuandaa na kutekeleza mipango mikakati mabali mbali kwa lengo la kuhakikisha
shughuli za utalii zinasambaa nchi nzima .
Makamu wa Rais amasema katika kuendeleza utalii kanda ya kusini,
ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea mkopo mwenye
masharti nafuu Dola za kimarekani milioni 150 kutoka benki ya Dunia ambapo
mradi huo utatekelezwa kwa miaka 6 kuanzia 2017/2018.
Mradi huo wenye lengo kuu la kukuza utalii
na kipato kwa wananchi kwa kuboresha miundo mbinu, kujenga uwezo katika
usimamizi wa maliasili na kuwawezesha wananchi wanaozunguka hifadhi kuzalisha
kwa tija
“Kama
nilivyosema hapo awali mradi huu utajulikana
kama Resilient Natural Resource for Tourism and Growth (REGROW)
na utaanza kutekelezwa katika maeneo ya hifadhi ya Taifa za Ruaha,
Mikumi, Udzungwa na Pori la Akiba Selous “
Makamu wa Rais ameiagiza Baraza la
Mazingira lililokuwa chini ya Ofisi yake kuharakisha tathmini ya mazingira ya
bonde la mto ruaha mkuu ili kuhakikisha kuwa mradi huu unatekelezwa kwa ufanisi
bila athari zozote baadaye za mazingira.
Makamu wa Rais alielekeza taasisi zote
zinazohusika zikiwemo Sekretarieti za
mikoa, Halmashauri za Wilaya na Vijiji kutoa ushirikiano wa kutosha wa kufanikisha utekelezaji wa shughuli za mradi.
“Tuhakikishe
sheria zinafuatwa na hakuna uvamizi wala shughuli za binadamu kwenye vyanzo vya
maji na hifadhi. Wahenga wanasema tunza mazingira yako yakutunze”.
Makamu wa Rais aliwashukuru benki ya Dunia
kwa kukubali kukopesha mkopo wenye masharti nafuu .
Aidha kabla ya Makamu wa Rais kuzungumza,
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla alisema Sekta ya
Utalii ni moja ya sekta za kipaumbele katika uchumi wa Tanzania ambapo
takribani asilia 20 ya pato la Taifa linatokana na utalii na robo ya fedha za
kigeni zinatokana na Utalii.
Kigwangala alisema
kuwa mradi huo utatekelezwa kwa miaka 6 lengo la mradi ni kukuza utalii
na kipato cha wananchi kwa kuboresha miundombinu
,kujenga uwezo katika usimamizi wa maliasili na kuwezesha
wananchi wanaozunguka hifadhi kuzalisha kwa tija.
‘Mradi utaongeza fursaza utalii na kuongeza
fursa za kiuchumi za wananchi wanaokaa
karibu na kupunguza migogoro baina ya wananchi.Alisema Kigwangala na kuongeza
kuwa
Mradi wa
Regrow utaanza kutekelezwa katika hifadhi ya Taifa
ya Ruaha ,mikumi , Udzungwa na pori la akiba la Selous
(kanda ya kasikazini ya Soleus kunakofanyika utalii wa
picha.
Mradi huu ni
sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Seriakali ya awamu ya Tano katika kufungua maeneo ya vivutio vya utalii
kanda ya kusini,hivyo mradi utaimarisha usimamizi wa utalii,utaimarisha
usimamizi wa maliasili,utaboresha maisha ya wananchi kwa kuboresha shughuli za kiuchumi za wananchi’Alisema Kigwangala
na kuongeza kuwa
Mheshimiwa
Makamu wa Rais kupitia Mradi wa Regrow Serikali itaimajenga na kuimarisha
miundombinu ya barabara,viwanja vya ndege,vituo vya ulinzi vya wanayamapoli na
kuimarisha ulinzi katikamageti ya kisasa yakuingia hifadhini katika hifadhi ya
Taifa ya Ruaha,Mikumi uzungwa na poli la akiba la Soleus
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla kabrasha lenye Andiko la mradi wa REGROW na Mikataba ya Fedha na utekelezaji wa mradi mara baada ya kuuzindua mradi huo katika eneo la Kihesa Kilolo mkoani Iringa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania (REGROW) ,Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
Waziri wa maliasili na utalii Hamisi Kigwangala akizungumza
wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania (REGROW) ,Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
Waziri wa maliasili na utalii Hamisi Kigwangala akizungumza
wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania (REGROW) ,Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya mpango wa uwekezaji katika miundo mbinu ya mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kabla ya kuzindua mradi wa REGROW.
0 maoni:
Chapisha Maoni