Ijumaa, 2 Februari 2018

DC KASESELA; TAASISI ZOTE MANISPAA YA IRINGA ZIGAWIWE MAENEO YA KUPANDA MITI KATIKA ENEO LA KIHESA KILOLO

Posted by Esta Malibiche on FEBRUARI 2,2018 IN NEWS
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akipanda mti katika eneo la Kihesa Kilolo mapema leo hii wakati wa uzinduzi wa upandaji miti  uliofanyia leo hii katika Mnaispa ya Iringa.Aliye mbele yake ni Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe.PICHA NA TUKUSWIGA MWAISUMBE

Na Esta Malibiche
Iringa
MKUU wa Wilaya ya Iringa,Richard Kasesela amewaongoza wanairinga katika zoezui la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Kihesa Kilolo Manispaa ya Iringa

Mkuu wa wilaya na viongozi mbalimbali akiwemo Meya, Mkurugenzi na viongozi wa Taasisi mbalimbali zilizopo katika Halmashauri ya Iringa Mjini wamepanda miche 100 katika eneo hilo.

Akizungumza na wananchi mara baada ya zoezi la uopandajui miti kukamilia, Mkuu wa Wilaya Richard Kasesela aliwataka wananchi wa Kihesa kilolo na Manispaa kwa ujumla kuitunza miti hiyo ili iweze kuleta manufaa nma si vinginevyo.

''Ninawaomba wanakihesa Kilolo kila mmoja awe mlinzi katika eneo hili ili tutakapokuja tena kukagua maendele tuikute miti yote tuliyoipanda leo imestawi.Kwa atakayebainika anafayana uzi akamatwe afikishwe kwenye vyombo vya dora''' Alisema Ksesela

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya amepiga marufuku shughuli za kilimo na uchimbaji mchanga katika eneo hilo na kuagiza Taasisi zote zigawiwe maeneo ya kupanda miti katika eneo hilo.
Mkurungenzi wa Manispaa ya Iringa akipanda mti.

Mejeja wa kiwanja cha Ndege Mkao wa Iringa akipanda mti.


 



0 maoni:

Chapisha Maoni